Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akionesha kitabu
chenye mwongozo wa Sera ya Wizara yake.
Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na
kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha
utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali
na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.
Katika
utekelezaji huu, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana lakini pia zipo
changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utoaji wa huduma za afya hapa
nchini.
Baadhi ya changomoto hizo ni za kiutendaji zaidi ambazo zinaweza
kutatuliwa kwa haraka endapo tutaimarisha usimamizi na uwajibikaji katika kila
ngazi kuanzia ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za
afya.
Changamoto hizi ni pamoja na wagonjwa kutopatiwa huduma haraka na sahihi,
lugha na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma na makundi yanayotakiwa kupata
matibabu bure (yaani Wazee, Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya miaka 5)
kutozwa fedha kinyume na Sera ya Afya ya 2007).
Takribani
kila siku vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio kadhaa kuhusu
malalamiko na kero mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi katika kupata huduma
za afya.
Wasimamizi
wa Wakuu wa Utekelezaji wa Sera na Miongozo ya Afya katika ngazi ya Mikoa ni
Waganga Wakuu wa Mikoa. Ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya
pamoja na kuhakikisha malalamiko na kero zao zinashughuhulikiwa kwa haraka,
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
(Mb) ameamua kuweka wazi namba za simu za Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO) wote
nchini ili wananchi wanapokuwa na malalamiko/kero waweze kuwasiliana nao moja
kwa moja.
Mhe Waziri
amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuyafanyia kazi masuala yote yanayoletwa na
wananchi katika Mikoa yao na kuyapatia ufumbuzi haraka. Hivyo, wananchi
wasisite kuwasiliana nao kupitia namba zao zifuatazo pamoja na kwa barua pepe.
Katika
muktadha mzima wa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Sheria na
Sera za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, mwananchi
yoyote ambae ana malalamiko, maoni au ushauri kuhusu sekta husika unaweza
kuwasiliana moja kwa moja na Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (Mb) kupitia simu
namba 0746 – 505030 (kwa njia ya ujumbe) pamoja na kueleza mkoa uliopo, twitter
@wamjw na email: waziri@moh.go.tz
“Uwazi na
Uwajibikaji ni chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya, sambamba na
kulinda Haki za Watoto, Wazee na Wanawake”.
MAWASILIANO
NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA (RMOs)
|
No comments:
Post a Comment