|
Serikali
yajipanga kupunguza ajali za barabarani kwa kiwango cha takribani asilimia 10
hapa nchini ili kupunguza vifo na majeruhi.
Akizungumza
Jana,Agosti 04,2016, jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Yusuf
Hamad Masauni kuwa baraza la Usalama
Barbarani linakerwa sana na kadhia ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa
zikitokea mara kwa mara.
“Kukithiri
kwa ajali za barabarani kwa siku za hivi karibuni, umewezesha Baraza kuibuka na
Mkakati wa Miezi Sita (6) unaolenga katika kukabiliana na ajali za barabarani
nchini, mkakati huu ni wa muda mfupi kuanzia mwezi Agosti, 2016 hadi Februari 2017 tutakapokaa na kutathmini
matokeo yake”, alisema Masauni.
Masauni
amesema ajali za barabarani zimewaacha watoto wakiwa yatima na kuwafanya akina mama kuwa wajane,
hivyo juhudi za makusudi inabidi
zifanywe ili kupunguza kama sio kuondoa kabisa ajali hizo.
Ametaja
vyanzo vikuu vya ajali za barabarani nchini kuwa ni pamoja na Makosa ya
Kibinadamu, mazingira ya barabara na ubovu wa vyombo vya moto.
Naibu waziri
huyo amesema takwimu za ajali barabarani katika miaka mitatu tangu 2012 ajali
ziliongezeka toka 23,578 hadi 23, 842 kwa mwaka 2013, vifo vilikuwa 3,969 kwa
mwaka huo hadi kufikia 1,043 mwaka 2013.
Vifo hivyo
vilipungua hadi kufikia 3,760 mwaka 2014, upungufu huo ulitokana na usimamiaji
madhubuti wa Sheria na kanuni za Usalama barabarani pamoja na juhudi
zilizofanya na Baraza kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Kwa mujibu
wa Masauni, Mkakati uliozinduliwa unalenga kudhibiti makosa yanayosababisha
madhara makubwa na ambayo husababisha kuongezeka kwa ajali za barabarani.
Ameyataja
mambo hayo kuwa ni:-
1. Udhibiti wa madereva walevi na kuendesha
kwa uzembe.
2. Udhibiti
wa mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa magari; kuwa na madereva wenza
3.
Uendeshaji magari bila sifa/leseni ya udereva na bima
4. Udhibiti
wa usafirishaji wa abiria kutumia magari madogo yenye muundo wa tairi moja
nyuma kwa mfano; Noah, Probox
5. Kudhibiti
ajali za pikipiki za magurudumu mawili ‘bodaboda’ na magurudumu matatu
6. Abiria
kufunga mikanda ya usalama wanapotumia vyombo vya usafiri
7. Kuyabaini
na kuyadhibiti maeneotete na hartarishi ya ajali za barbarani ‘black
spots/kilometers’
8. Kuangalia
uwezekano wa kufanya marekebisho ya sheria za usalama barabarani.
9. Kuanza
kwa mfumo wa nukta ‘point system’ kwenye leseni za udereva.
10. Kutoa
mafunzo ya msasa yanayolenga katika kuimarisha utendaji wa askari wa usalama
barabarani.
11.
Kuhakikisha kuwa waendesha bodaboda wanafikiwa na kupewa mafunzo yaa uhakika
juu namna na jinsi ya kuzitumia barabara kwa usalama zaidi.
12.
Kudhibiti rushwa na kuwaadhibu watoaji na wapokeaji wa rushwa katika barabara
zetu nchini.
13.
kuwahusisha wamiliki wa magari ya abiria na ya mizigo, katika kuutekeleza
mkakati.
14. Mkakati
mwingine waliouweka ni kuwa Dereva ukikamatwa unapelekwa rumande na baadae
mahakamani kujibu shitaka litakalokuwa linakukabili.
|
No comments:
Post a Comment