Watumishi waliotajwa walihusika kufanya yafuatayo kila mmoja kulingana
na nafasi aliyokuwepo kama msimamizi mkuu wa eneo hilo, Kwanza ni kufanya Mabadiliko ya mkataba wa Ujenzi wa kituo cha
Mabasi (Bus Stand) ya Kemondo (Tshs 44 milion) bila idhini ya Bodi ya zabuni ya
Halmashauri kinyume na Kanuni za
Manunuzi kanuni ya 110 (5).
Pili,
kulipa Mishahara kiasi cha Tshs 28,072,549/=
iliyolipwa kwa Watumishi hewa (watoro na waliostaafu ) wakiwemo
watumishi wa idara ya Elimu Sekondari
ambapo, kutokana na uzembe wa Afisa Elimu Sekondari Wilaya na Afisa Utumishi wa
Wilaya (2014/2015) kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kukagua na kuchukua
hatua za kuwaondoa watumishi wasiostahili kulipwa kwa wakati katika orodha ya malipo (Payroll),
walisababisha Serikali kupata hasara ya Tshs 28,072,549/= na kuzilipa taasisi
mbalimbali za fedha makato hewa ya kisheria kiasi cha Tshs 9,811,947.55
Tatu, Kubadili
matumizi ya fedha za ujenzi wa daraja la Kyamabale kiasi cha Tshs 200,000,000/=
bila kuzingatiwa taratibu za kubadili matumizi ya fedha za maendeleo na kusababisha
kutokamilika hadi sasa, ujenzi wa daraja lililolengwa kuondoa kero kwa wananchi
halijakamilika na lilitakiwa kukamilika tarehe 26 Oktoba, 2015.
Nne, Manunuzi
ya vifaa tiba na madawa ya Hospitali Tshs 16,339,050/= kufanyika bila dihini ya Bodi ya zabuni 2009/2010. Hoja
hiyo ilitokana na baadhi ya watumishi kutoheshimu sheria na miongozo ya
Serikali kwa kisingizio cha dharura.
Tano, Manunuzi
ya mafuta ya thamani ya Tshs 12,789,364 (mwaka 2013/14) ambayo kwa sasa ni sawa
na lita 6,394 ambayo yangewezesha gari moja kusafiri umbali wa kilometa 31,973.
Mafuta hayo pamoja na kulipiwa na Halmashauri, hakuna uthibitisho kuwa
yalipokelewa katika vitabu vya kupokea mali za Halmashauri na hakuna udhitisho
wa matumizi yake.
Haya ni manunuzi hewa.
Sita, Kesi
za mapato ya Halmashauri zilizokwishatolewa maamuzi na Mahakama na ilipaswa
kutekeleza hukumu kupitia Mwanasheria wa Halmashauri. Zaidi ya Tshs
14,800,000/= za Halmashauri hazijafuatiliwa kwa kutekelezwa ama kukaza hukumu
na mwanasheria wa Halmashauri. Saba, Matumizi ya Tshs 7,150,000/= za mapato ya
ndani bila kufuata taratibu za fedha na hakuna nyaraka zozote zilizoidhinisha na kuthibitisha matumizi ya fedha hizi ambazo
zilipokelewa na mtunza fedha.
Mwisho, Ujenzi
wa ofisi ya Afisa Elimu (Sekondari) Tshs 59,500,000/=. Ofisi hii imekamilika
lakini haitumiki kwa sababu fedha zote
zilitolewa na Serikali lakini Mkandarasi
hajalipwa. Hii inaongeza deni la Halmashauri kwa mujibu wa mikataba kwa sababu
fedha zilibadilishwa matumizi bila idhini ya Mamlaka.
“Kutokana
na ukiukaji wa sheria za usimamizi wa watumishi, udhaifu katika usimamizi wa
fedha na manunuzi, Mkurugenzi na Baraza la Madiwani wachukue hatua za kinidhamu
mara moja na kuniletea taarifa ya utekelezaji wa agizo langu ifikapo tarehe 30
Agosti, 2016.” Aliagiza Mhe. Kijuu.
|
No comments:
Post a Comment