MIAKA 80 YA SIMBA SC:-Wageni AFC Leopars wapigwa 4-0 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, August 08, 2016

MIAKA 80 YA SIMBA SC:-Wageni AFC Leopars wapigwa 4-0 .

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC imeadhimisha miaka 80 ya kuanzishwa kwake kwa ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya AFC Leopards toka Kenya mchezo uliopigwa leo Agosti 08,2016 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba SC ilionekana kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa ambapo dakika ya 38 Ibrahim Ajib aliipatia Simba bao la kuongoza baada ya kupokea pasi safi toka kwa Jonas Mkude na kuachia shuti la chini chini la mita 25.

Kipindi cha pili Simba SC iliwaingiza Muzamir Yassin, Jamal Mnyate na Laudit Mavugo ambao walibadilisha mchezo kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza mashambulizi na kuwafanya mabeki wa Leopards kuwa 'bize' muda wote.
Dakika ya 55 Ajib tena aliifungia Simba SC goli la pili baada ya Mavugo kuichambua safu ya ulinzi ya Leopards na kumrahisishia mfungaji.

Dakika kumi baadae Kichuya alifungia Simba SC goli la tatu baada ya kupokea mpira wa krosi uliopigwa kiufundi na Mavugo.

Mavugo ndiye aliyehitimisha karamu ya magoli baada ya kumalizia kazi kubwa iliyofanywa na Kichuya ambaye aliwafanya mabeki wa Leopards kuwa nae macho muda wote.

Mashabiki wa Simba SC waliohudhuria mchezo huo wameonesha imani kubwa kwa kikosi chao kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha wanandinga wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad