|
Akizindua
mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Veta Mkoani Kagera kilichopo katika
Manispaa ya Bukoba,Mkoani Kagera, Mhandisi Manyanya aliwapongeza walimu waliohudhuria awamu ya
kwanza ya mafunzo hayo yaliyoanza Agosti 1, 2016 kutoka katika Halmashauri za
Wilaya za Karagwe na Bukoba kwa kuitikia wito wa mafunzo hayo kwa asilimia 99%.
Pia
aliwasistiza walimu hao kuzingatia mafunzo kwa umakini kwani lengo la Serikali
ni kuhakikisha walimu hao wanatoa elimu bora kwa wanafunzi ambapo mwanafunzi
yeyote hawezi kupata elimu iliyobora kama hajui kusoma, kuandika na kuhesabu
(KKK) masomo ambayo ndiyo msingi wa kujifunza.
Mhandisi
Manyanya alisema kuwa mafunzo ya (KKK) yanaendeshwa katika mikoa 19 ya Tanzania
Bara na jumla ya walimu 22995 watapatiwa mafunzo hayo ukiwemo Mkoa wa Kagera
utakaonufaika kwa mafunzo hayo kwa walimu 1770 ambao wanatarajiwa kuwanufaisha
pia walimu wenzao kwa mafunzo hayo ya (KKK) pindi warejeapo shuleni kwao.
Ombi,
Mhandisi Manyanya aliwaomba walimu hao pia kuanzisha madarasa ya watu wazima
ili kutoa fursa kwa wananchi ambao hawakuweza kupata elimu ya msingi ili na wao
wafundishe kusoma, kuandika na kuhesabu. “Kwa takwimu za Sensa ya mwaka 2012
ilionekana kuwa bado asilimia 29% ya wananchi kuanzia umri wa miaka 8 hadi 50
hawajui kusoma na kuandika kwahiyo nawaombeni sana tusaidiane kuondoa tatizo
hili nchini kwetu.” Aliwaomba walimu hao Mhandisi Manyanya.
|
No comments:
Post a Comment