LIGI KUU ENGLAND 2016/2017:-Arsenal walizwa kwao 4-3. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 14, 2016

LIGI KUU ENGLAND 2016/2017:-Arsenal walizwa kwao 4-3.

Uwanja wa Emirates Jijini London ulikuwa na sherehe ya Magoli baada ya Bao 7 kutumbukizwa wakati Liverpool  ikishangilia ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya wenyeji, Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza 2016/2017 ,leo Agosti 14,2016.


 Mabao ya Liverpool yamefungwa na Phillippe Coutinho dakika ya 46, 56 ,Adam Lallana  dakika ya 49 na Sadio Mane dakika ya 63  wakati ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott  dakika ya 31,Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 64 na Calum Chambers dakika ya 75.

Ligi Kuu Uingereza inaendelea Jumatatu,Agosti 15,2016 Usiku kwa Mechi moja kati ya Chelsea na West Ham United huko Stamford Bridge.

Nao Manchester United waliitandika Bournemouth Bao 3-1 na kuamsha shangwe za Mashabiki wao kuimba 'Jose Mourinho' mwishoni mwa Mechi.

Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 40 baada ya pasi ndefu ya Ander Herrera kuwahiwa na Beki wa Bournemouth Simon Francis ambae alitoa nyuma kumrudishia Kipa wake Boruc lakini Juan Mata akainasa na Kipa Boruc kuokoa na Mpira kumgonga Simon Francis na kurudi tena kwa Mata aliefunga kilaini.

Dakika ya 59 Kepteni Wayne Rooney akapiga Bao la Pili kwa Kichwa baada ya Krosi ya Valencia kuunganishwa fyongo na Anthony Martial na kumkuta Rooney aliemalizia hadi wavuni.

Bao la 3 la Man United lilipachikwa na Mchezaji Mpya Zlatan Ibrahimovic katika Dakika ya 64 na kuwa Bao lake la kwanza kwa Klabu yake mpya.

Adam Smith aliipa Bournemouth Bao lao pekee Dakika ya 64 na Mechi kwisha kwa Bournemouth kufungwa bao 1-3 na  Man United .
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad