CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-TP Mazembe yalizwa 3-2…Yanga SC sasa mguu nje Nusu fainali. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 14, 2016

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-TP Mazembe yalizwa 3-2…Yanga SC sasa mguu nje Nusu fainali.

Mabingwa wa Tanzania Bara ,Yanga SC unaweza sema kuwa rasmi wameaga Mashindano ya KOMBE LA SHIRIKISHO la CAF baada ya Timu ya Medeama ya Ghana kuichapa TP Mazembe  magoli 3-2  katika Mechi ya Kundi A.

Bao liloiua TP Mazembe hii Leo,Agosti 14,2016 lilifungwa Dakika ya 90 na Kwesi baada ya Medeama kutangulia 2-0 kwa Bao za Eric Kwakwa na Sarborg, Dakika za 32 na 60, na TP Mazembe kusawazisha Dakika za 61 na 73 kwa Bao za Bolengi na Kalaba.

 Huku kila Timu ikibakiza Mechi moja, TP Mazembe, wakiwa na Pointi 10, tayari wametinga Nusu Fainali na kuiacha Nafasi ya Pili kusonga kugombewa na Medeama na MO Bejaia ya Algeria ambao Jana, Agosti 13,2016, Jumamosi walifungwa 1-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na Yanga SC.

Medeama wanashika Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 8 na MO Bejaia wakiwa na Pointi 5 na mkiani wako Yanga SC wenye Pointi 4.

Mechi za mwisho ni hapo Agosti 23,2016 wakati Yanga SC wapo huko Lubumbashi Congo DR kukamilisha ratiba na TP Mazembe wakati MO Bejaia wako kwao kucheza na Medeama.

Kundi B limebakisha Mechi moja tu na tayari FUS de Rabat ya Morocco na ES Sahel ya Tunisia zimeshatinga Nusu Fainali.23


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad