Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe, Ummy Mwalimu amewapongeza USAID kwa kufadhili mradi wa Jhpiego wa Afya ya
Mama na Mtoto (MCSP) ambao umewezesha utolewaji wa mafunzi na kujengewa uwezo
wahudumu wa afya wanaotoa huduma kwa kina mama, watoto wachanga, na watoto
chini ya miaka mitano ikijumuisha wale wanaofanya kazi katika hospitali hiyo.
Ukarabati na upanuzi wa wodi ya wazazi ulianza mwezi Oktoba
mwaka jana,2015 na kukamilika mwezi Machi mwaka huu,2016 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi
iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jhpiego, Dkt. Leslie Mancuso.
Upanuzi wa
jengo hilo umewezesha ongezeko la vitanga kwa ajili ya kulaza akina mama
wajawazito na wale waliojifungua na ambao wanahitaji uangalizi.
Upanuzi huo umeongeza idadi ya vitanda kutoka 28 hadi
66 na pia kuongeza vituo vya wauguzi katika wodi hiyo ya wazazi pamoja na vyoo.
Jumla ya gharama zilizotumika ni jumla ya Tshs. 136,532,166.92 (Milioni mia
moja na thelathini na sita, laki tano na thelathini na mbili elfu, mia moja
sitini na sita na senti tisini na mbili).
|
No comments:
Post a Comment