WAZIRI NAPE - Ukinunua CD isiyo na stika, wewe ni mwizi kama wezi wengine na Utashughulikiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 16, 2016

WAZIRI NAPE - Ukinunua CD isiyo na stika, wewe ni mwizi kama wezi wengine na Utashughulikiwa.

Waziri Nape akitoa CD fake Madukani,Jana July 15,2016.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wa Tanzania, Mhe. Nape Nnauye baada ya kufanya ziara Jana Ijumaa,July 15,2016 katika maeneo ya Kariakoo, Jijini Dar es Salaam kukagua na kukamata CD ambazo hazina stika ya TRA, amewataka Watanzania kuacha tabia ya kukunua CD ambazo hazina stika za TRA.

Akiongea na waandishi wa Habari katika msako huyo, Waziri Nape amesema yeyote anayekamatwa na CD ambao haina stika ya TRA atashtakiwa kwa kosa la kuhujumu uchumi.

Kila anayenunua sasa kazi ya sanaa ambayo haina stika ya TRA naye ni mwizi kwa kama mwizi yoyote sababu ameshirikiana na muuzaji ambaye hajalipa kodi, hata tukikukuta na CD moja haina stika wewe ni mwizi kama mwizi mwingine tutashughulika na wewe,” alisema Nape.

Katika ziara hiyo zaidia ya maduka 40 yamefungwa huku CD fake zikichukuliwa kwa ajili ya kuharibiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad