|
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu Pro. Faustine Kamuzora akiongea na mmoja
wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani mara baada ya kusaini saini
makubaliano kwa ajili ya kuunganisha kufikiwa kwa intaneti katika shule za
sekondari nchini ili kuwezesha elimu kielektroniki shuleni katika hafla
iliyofanyika shuleni hapo mapema jana,Julai 13,2016.
Kampuni inayoongoza kwa mtindo
wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania Jana Julai 13,2016, imeingia ubia na Wizara ya
Mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu katika kuwezesha kufikiwa kwa intaneti
katika shule za sekondari nchini ili
kuwezesha elimu kielektroniki shuleni
katika zoezi ambalo litachukua miaka miwili.
Kama sehemu ya
makubaliano hayo, wizara itabainisha na kutoa orodha ya shule zisizo na maabara za kompyuta ili
ziunganishwe na hali kadhalika kuongoza
utekelezaji wa mradi wakati Tigo itadhamini
maendeleo ya miundombinu katika shule nchini ikiwa ni pamoja na kuunganisha
nyaya ndani ya madarasa na kufunga
visivyotumia nyaya (LAN) na vituo vinavyofikia
mtandao wa intaneti.
Alipokuwa akisaini makubaliano hayo katika
Shule ya Sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Biashara wa
Tigo, Shavkat Berdiev, alisema, “Kupitia Idara yetu ya huduma kwa jamii hivi
sasa tunatekeleza dira ya serikali ya kuibadilisha nchi kuingia katika uchumi
uliojikita katika uelewa ifikapo mwaka 2025 na kampuni yetu imejipanga kuhakikisha shule nyingi za sekondari Tanzania zinafikiwa na mtandao wa intaneti.
“Tunajivunia
kushirikiana na Wizara ya mawasiliano, Ujenzi na Miundombinu katika kuwezesha vijana na jamii kwa ujumla kuingia katika mkondo wa kidunia wa habari na uelewa, ambako watajifunza, kupanua uelewa
wao na kushirikiana na wenzao katika sehemu mbalimbali duniani.”
Berdiev aliongeza
kusema, “Tigo itaendelea kufanya kazi na
serikali katika miradi mingine ya ubunifu na inayovutia ili
kunyanyua maisha ya Watanzania walio wengi”.
Akiishukuru Tigo wakati
wa kusaini makubaliano hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Ujenzi na
Miundombinu Pro. Faustine Kamuzora alisema, “Ni kupitia ushirikiano kama huu
ndipo tutaweza kusambaza stadi za kisasa za Tehama pamoja na uelewa kwa vijana
ili kuwawezesha kukabiliana na
changamoto zinazotokana na mtiririko wa
mabadiliko ya habari ya kila siku ndani ya jamii na katika uchumi wa dunia.”
Prof. Kamuzora
aliongeza, “Naipongeza Tigo kwa utayari wake wa kujingiza katika makubaliano
baina ya sekta binafasi na sekta za umma ili kuwasaidia wanafunzi wa shule za
sekondari nchini Tanzania na vile vile tunakaribisha wadau wengine kushiriki kuunganishwa kwa teknolojia hii.
Mradi wa kielektroniki
mashuleni (eSchools) ni moja ya miradi mkakati ya uwekezaji kijamii ya Tigo na
hadi sasa Tigo imeweza kuunganisha shule 31 za sekondari za serikali na
mtandao wa intaneti ikiwa na mpango wa baadaye wa kuziunganisha shule 50 kwa mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment