Takwimu kuhusu Mikoa Mitano masikini
zaidi nchini Tanzania, zimezidi kuzua mjadala Bungeni huku Wabunge wakizitumia
kutaka misaada zaidi katika mikoa yao na wengine wakidai zinawafanya wahofu
kwamba kuna ajenda ya siri kwani hawaamini usahihi wake.
Katika mjadala wa Jana,June 16, 2016, kuhusu Bajeti inayopendekezwa na Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017,Mbunge wa Nyamagana mkoa wa Mwanza, Mhe.Stanslaus Mabula (CCM), alitumia takwimu hizo kutaka serikali kuanza kwa kuupa mkoa huo Sh milioni 50 zilizoahidiwa katika kila kijiji ili wananchi wa mkoa huo wapunguze ‘umasikini wao’.
“Ninaomba hizi shilingi milioni 50, zianzie katika
mikoa iliyoainishwa kuwa masikini kwa mujibu wa takwimu za waziri ukiwemo mkoa
wangu wa Mwanza,” alisema Mabula.
Alisema
kwa Tanzania msingi mkubwa wa kuondokana na umasikini ni kilimo na maeneo ya
kulima yapo, ndio maana Serikali inasema ‘Hapa Kazi Tu’ ili watu wajikite katika
kilimo......BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.Naye Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Mhe.Jason Rweikiza alitumia takwimu hizo kutaka serikali kuwaondolea wakulima wa kahawa kodi 26 wanazolazimika kulipa pamoja na kudhibiti ugonjwa wa mnyauko unaoshambulia migomba ili kuwaokoa wananchi wa Kagera na umasikini. “Kahawa inakatwa kodi 26, kwa nini wananchi wasiwe masikini? Migomba inaelekea kumalizika kabisa kwa sababu ya ugonjwa wa mnyauko, kwa nini wananchi wasiwe masikini,” alisema. Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe.Maria Kangoye anayewakilisha mkoa wa Mwanza alipinga takwimu zinazoonesha kwamba mkoa huo ni miongoni mwa mikoa mitano masikini nchini. Alisema takwimu za Benki Kuu (BoT) zinaonesha kwamba Mwanza ni mkoa wa pili nyuma ya Dar es Salaam katika kuchangia kwenye Pato la Taifa. Akiwasilisha Bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi ya Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alitaja mikoa masikini zaidi kuwa ni Kigoma, Geita, Kagera, Singida na Mwanza; wakati mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Pwani na Manyara ndiyo mikoa mitano yenye ahueni ya umasikini nchini. Akiuliza swali la papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ,Jana,June,16,2016, Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Mhe.Oscar Mukasa (CCM), alisema utafiti kuhusu kipato cha kaya, umebaini mikoa mitano inayokabiliwa na umasikini uliokithiri na kumtaka Majaliwa kueleza serikali itafanya nini katika mikoa hiyo ili iondokane na aibu wakati ina fursa za kiuchumi ikiwemo kilimo cha pamba, mibuni na michikichi. Waziri Majaliwa alisema serikali haijaacha jambo hilo kama lilivyo, bali imekuwa ikishawishi wananchi kujianzishia miradi na wengine waunde vikundi, ikiwemo vya Vicoba ili kujijengea mtaji wa pamoja ili waanzishe miradi hiyo. |
Friday, June 17, 2016
MIKOA MASIKINI TANZANIA:- Wabunge waijadili Takwimu na uligawa Bunge.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment