MATOKEO / RATIBA EURO 2016:-Italia waungana na Ufaransa 16 Bora huku Czech Republic na Croatia sare. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 17, 2016

MATOKEO / RATIBA EURO 2016:-Italia waungana na Ufaransa 16 Bora huku Czech Republic na Croatia sare.

Timu ya Taifa ya Italia,leo June 17, 2016,Wamefanikiwa kwenda Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku wakiwa na Mechi 1 mkononi baada ya kuichapa Sweden bao 1 - 0 huko Stadium de Toulouse Mjini Tolouse, Ufaransa kwa Bao la Dakika ya 88 katika Mechi ya Kundi E la la EURO 2016.
Bao hilo lilifungwa baada ya Mpira wa kurushwa na Giorgio Chiellini Kuguswa kwa Kichwa na Simone Zaza, alieanzia Benchi, na Éder Eder Citadin Martins na kuwatoka Wachezaji Watatu wa Sweden na kufunga.
Matokeo ya mchezo mwingine wa leo June 17, 2016, Czech Republic Pichani,wametoka sare ya bao 2 – 2 na  Croatia.

Alhamisi Juni 16, 2016.

KUNDI B, England 2 -1 Wales

KUNDI C, Ukraine 0 – 2 Northern Ireland

KUNDI C, Germany 0 – 0 Poland

Ijumaa Juni 17, 2016.

KUNDI E, Italy 1 – 0 Sweden

KUNDI D, Czech Republic 2 - 2 Croatia

KUNDI D, Spain v Turkey (2200, Stade de Nice)

Jumamosi Juni 18, 2016.

KUNDI E, Belgium v Republic of Ireland (1700, Stade de Bordeaux)

KUNDI F, Iceland v Hungary (1900, Stade Velodrome, Marseille)

KUNDI F, Portugal v Austria (2200, Parc des Princes, Paris)

TIMU ZILIZOFU KUINGIA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16.

-KUNDI A: Ufaransa

-KUNDI E: Italia

**Bado Timu 14

**Washindi Wawili wa juu wa Kila Kundi na Timu Bora 4 zilizomaliza Nafasi za Tatu zitaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16.


Matokeo haya yameiacha Sweden, ambao walitoka 1-1 na Republic of Ireland, kuhitaji kuifunga Ubelgiji katika Mechi yao ya mwisho ikiwa watataka kuwa na matumaini yeyote ya kufuzu kutoka Kundi E.

Nao, Italia, ambao walianza Kundi E kwa kuifunga 2-0, wamesonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku wakibakisha Mechi 1 na Republic of Ireland.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad