Serikali ya Tanzania, imepitisha
bajeti ya shilingi trilion 29.5 kwa kupigiwa kura huku Wabunge wa Upinzani
wakiwa wametoka nje wakiwa wameziba midomo yao kwa karatasi na plasta ikiwa ni
ishara ya kuonesha kutoridhika na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson wakigomea vikao
vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika huyo.
Katika vikao vya Bunge la 11, Wabunge
wa Vyama vya Upinzani wamekuwa wakisusia vikao hivyo kwa takribani siku 23 sasa
kwa madai ya kutokubaliana na ukandamizaji unaofanywa na Naibu Spika wa Bunge
Dkt.Ackson Tulia.
Wakichangia bajeti hiyo, Waziri wa
Nishati na Madini Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo pamoja na Waziri wa Viwanda
na Biashara Mhe.Charles Mwijage wamesema bajeti hiyo inalenga kukuza uzalishaji.
Akijibu hoja mbalimbali za Wabunge
waliochangia katika Bajeti hiyo ikiwa ni pamoja na ya kuongeza fedha katika
ofisi ya mkaguzi wa serikali CAG ili kutanua wigo wa ukaguzi pamoja na kuachana
na mpango wa kuanza kuwakata kodi wabunge katika mafao ya kiinua mgongo ya
Wabunge, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema msimamo wa
serikali upo pale pale.
Kuhusiana na makato ya kodi kwenye
mafao ya wabunge, Dkt Mpango amesema kuwa serikali imeamua kuwa itakata kodi
hiyo kwa viongozi wote wa kisiasa wakiwemo wakuu wa wilaya, wakuu wa mkoa,
Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais pia, ili kuweka usawa katika makato ya kodi
nchini.
Baadaye jioni wabunge walipiga kura
mmoja mmoja kupitisha bajeti hiyo, ambapo Wabunge wote 251 waliokuwemo bungeni
walipitisha bajeti hiyo kwa kauli moja, ambapo kila mbunge alijibu
"Ndiyo" akimaanisha anaipitisha bajeti hiyo.
Mapema Asubuhi mara baada ya dua, Wabunge wa Upinzani waliziba midomo yao kwa karatasi na Plasta na kutoka nje ya
ukumbi wa Bunge ikiwa ni ishara ya kuonesha kutoridhika na Naibu Spika wa Bunge
Dkt. Tulia Ackson.
Mbunge wa Vunjo Kupitia chama cha
NCCR Mageuzi, Mhe. James Mbatia kwa niaba ya wabunge hao alisema hawataacha
kulalamikia ukiukwaji wa sheria unaofanywa na kiti cha Naibu Spika... Endelea KUSOMA MAJIBU YA WAZIRI WA FEDHA KWA <<...KUBOFYA
HAPA..’’
|
Monday, June 20, 2016
Home
HABARI
SIASA
BAJETI KUU YA SERIKALI TANZANIA 2016/2017 :-Yapitishwa Bungeni huku Kodi ya Kiinua mgongo Itakatwa kwa Watumishi wote akiwemo Rais.
BAJETI KUU YA SERIKALI TANZANIA 2016/2017 :-Yapitishwa Bungeni huku Kodi ya Kiinua mgongo Itakatwa kwa Watumishi wote akiwemo Rais.
Tags
# HABARI
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment