Kwenye Dakika ya 105
, Chris Smalling alipewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Dakika ya 110, Jesse
Lingard alieingizwa Dakika ya 90 kumbadili Juan Mata alifunga Bao la ushindi
baada ya kazi nzuri ya Rooney.
|
Linakua ni Taji la kwanza kwa Meneja Van Gaal kutwaa
Taji lake la kwanza akiwa na Man United na pia kuipa Klabu hiyo Kombe la kwanza
tangu Sir Alex Ferguson astaafu Mei ,2013 ingawa mwanzoni mwa Msimu wa 2013 / 2014,
wakiwa chini ya David Moyes, walibeba Ngao ya Jamii walipoibwaga Man City.
|
DONDOO MUHIMU.
-Hii ni Mechi ya
Fainali ya 135 ya FA CUP.
-Fainali hii ni kama
Marudio ya Fainali ya Mwaka 1990 ambayo Manchester United waliifunga Crystal
Palace 1-0 baada ya Mechi ya kwanza kwisha Sare 3-3.
-Hii ni mara ya Pili
kwa Palace kutinga Fainali wakati kwa Man United ni Fainali ya 18 na wameshinda
11 kati ya hizo wakipitwa tu na Arsenal walioshinda Fainali 12
-Mara ya mwisho kwa Man
United kutwaa FA CUP ni Mwaka 2004 walipoifunga Timu ya Daraja la Kwanza
Millwall 3-0.
|
No comments:
Post a Comment