Rais Magufuli ametua katika uwanja wa
ndege wa Entebe majira ya saa tano za asubuhi na kupokelewa na Waziri wa Ujenzi
na usafirishaji wa Uganda Mheshimiwa John Byabagambi na kisha kuelekea Ikulu ya
Entebe ambako amepokelewa rasmi na mwenyeji wake Mheshimiwa Rais Yoweri Kaguta
Museveni.
Akiwa katika Ikulu ya Entebe Rais
Magufuli amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na pia
amepigiwa mizinga 21.
|
Aidha, Viongozi hao wamefanya
mazungumzo ambapo pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano na
uhusiano kati ya nchi hizo mbili, Rais Magufuli amemhakikishia Rais Museveni
kuwa Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha ujenzi wa bomba la
mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka Hoima katika Ziwa Albert nchini Uganda na
kupita kaskazini mwa Tanzania hadi bandari ya Tanga.
Rais Magufuli ameongozana na Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Mheshimiwa Suzan Kolimba.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU
Kampala
11 Mei, 2016
|
No comments:
Post a Comment