MOORLAND PREMIER HOTELS LIMITED
CCM/MURGWANZA ROAD – NGARA
S. L. P 223
NGARA – KAGERA
NORTH WESTERN OF TANZANIA
Email: mphngara@gmail.com
Simu: +255 787 370 633/786 803 878/754 979 868/758 421 849
01/05/2016
TANGAZO LA NAFASI ZA
KAZI (26)
Moorland Premier Hotels and Tours
Limited ni Hotel Mpya na ya Kisasa inayotaraji wa Kufunguliwa rasmi ndani ya
mwaka huu wa 2016 Msimu wa Mavuno (Fiesta time).
Iko katika hatua za mwisho kukamilika
na inatarajiwa kutoa ajira za kudumu na za muda kwa wazalendo na wageni
wasiopungua arobaini (40) ndani ya Wilaya ya Ngara na njeya Wilaya.
Hotel ipo Wilayani Ngara Karibu na
Kituo Cha Police/Magereza 0.5km Kutoka Barabara kuu (High way) ya kwenda
Kabanga/Burundi Boarder, Ofisi ya CCM, Barabara ya Murgwanza Hospital, Mkoani
Kagera, Kasikazini Magharibi nchini Tanzania.
Uongozi wa
Hotel unapenda Kuwatangazia Nafasi za Kazi Kama ifuatavyo:-
1. Hotel
Manager/Meneja wa Hotel - Nafasi (1)
2.
Mapokezi/Receiptionist (2)
3.
Wapishi/Cooks - Nafasi (4)
4.
Wahudumu/Bar & Kitchen Attendants – Nafasi (8)
5. DJ –
(Disco Joker/Mchezesha Mziki) – Nafasi moja (1)
6.
Walinzi/Security Guards – Nafasi Mbili (2)
7. Mtunza
Stoo/Store kepeer- Nafasi Moja (1)
8.
Wafanya Usafiwa Ndani/House Keepers/Washers – Nafasi tano (5)
9. Mfanya
usafiwa Mazingira/Garderner – Nafasi Moja (1)
10.
Mhudumu/Attendant M-Pesa (Vodacom, Airtel Money, Tigo Pesa, NMB, CRDB Bank na
RIFARO/Selcom) Wakala – Nafasi Moja (1)
Waombaji/Muombaji
wawe/awe na sifa zifuatazo Kiujumla:-
· Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa
kuanzia miaka kumi na nane (18yrs) na Kuendelea
· Awe na Hati ya Kuzaliwa ya Tanzania au
Kitambulisho cha Makazi yake
· Awe anajua kusoma na Kuandika Kiswahili,
Kiingereza au Kifaransa
· Awe na Elimuya Kuanzia Kidato Cha nne na
Kuendelea
· Awe hajawahi Kuhusika na kesi ya aina
yoyote ya Police ama Kufikishwa Mahakamani
· Awe Tiyari Kufundishwa na Kufundisha pale
inapobidi
· Awe Mbunifu na Mwenye Kujituma bila
kushurutishwa
· Awe
Mkarimu/Hospitality kwa wageni na Mwaminifu kwa Mwajiri wake
· Awe na uzoefu wa kazi kwa nafasi husika
kuanzia Miaka miwili (2) na Kuendelea
· Awe na Vyeti vya Uzoefu Kwenye Kazi
husika, Vyenye anuani na namba za simu au barua pepe za mwajiri wake sehemu
alipofanya kazi au anapofanya kazi kwa sasa
· Awe tiyari Kuwajibika au kuwajibishwa
pale inapobidi
Ngongeza ya sifa Kwa
Nafasi baadhi hapo Juu:
1.
Hotel Manager/Meneja wa Hotel/ Mapokezi/Receiptionists/Wahudumu/Bar
& Kitchen Attendants
· Awe Amehitimu masomo ya utawala wa Hotel
na Utalii/Hotel Management
and Tour
Guides na awe na cheti cha chuo kinachotambulika
· Awe amehudhulia Semina mbalimbali za
uongozi Shupavu na awe na vidhibitisho.
· Aliyesoma masomo ya Komputa na Anaye jua
Kutumia komputa atapewa kipa umbele zaidi
2.
Wapishi/Cooks
· Awe Amehitimu masomo ya utawala wa Hotel
na Utalii/Hotel Management and Tour Guides na awe na cheti cha chuo
kinachotambulika.
· Awe
amehudhulia Semina mbalimbali za Upishi na awe navidhibitisho
· Awe anajua Kutengeneza Menu ya Siku, ya
wiki na ya Mwezi
· Awe anajua kusoma na kuitafsiri Menu kwa
wateja/Wageni
3.
Kwa walinzi/Security Guards:
· Atakaye kuwa na cheti cha kuhitimu
mafunzo ya Mgambo au kozi yoyote ya ulinzi kwenye shule ama chuo
kinachotambulika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapewa
Kipaumbele.
4.
Mtunza Bustani/Garderner:
· Anayejua Kutumia vizuri na Kutengeneza
Mashineya Kukata Nyasi yenye injini ya Petrol atapewa kipaumbele
5.
DJ – Disco Joker/Mchezesha Mziki:
· Mwenye Vyeti Vya Chuo Cha sanaa na
Utamaduni kilichosajiliwa na BASATA (Baraza la Sanaa Tanzania) na Kutambuliwa
na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenye uzoefu kazini pia akiwa na
Tanzania Driving Licence atapewa Kipaumbele
6.
Mhudumuwa M-Pesa/M-Pesa Attendant:
· Aliyesoma masomo ya Komputa na Anaye jua
Kutumia komputa atapewa kipa umbele zaidi
Mwenye sifa zote hapo juu ataitwa
kufika kwenye Mchujo/Interview kupitia namba zake za simu au Barua Pepe atakazo
kuwa ametuandikia kwenye barua yake ya maombi.
Gharama za Usafiri wa kuja na kurudi
ulikotoka wakati wa mchujo/Interview Pamoja na za Chakula na Kulala ni za kwako
mwenyewe
Mwisho wa Kupokea Maombi ni Tarehe 25/5/2016 Saa nne (4:00) Asubuhi
Maombi yatumwe Kwenye Anuani Tajwa
hapo juu, au kwenye baruapepe ya mphngara@gmail.com au yafikishwe Paradise
Hotel/Restaurant – Nakatunga Ngara (TZ) na ya ambatanishwe na kopi za vyeti
vyako vya origino.
Ukituma maombi na ikafika tarehe
31/05/2016 Kabla haujaitwa au kupigiwa simu kwa namba yoyote kati ya hizo hapo
juu kwenye anuani yetu, Tafadhali usitupigie simu, tambua kuwa Barua yako na
vyeti vyako hatujaridhika navyo.
Moorland Premier Hotel itakua na
masilahi mazuri na malengo mazuri ya kukuza na kuendeleza vipaji vya wafanya
kazi kwa kupitia mafunzo mbalimbali kwa kazi husika.
– Mishahara ni makubaliono baada ya Mchujo.
|
No comments:
Post a Comment