Mbunge wa Ulanga,Mhe. Godluck Mlinga (CCM) ameyatuhumu mashirika ya umma ambayo
hayajajiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwa watendaji wake wakuu
wamepewa malipo ya asilimia 10 ili mashirika hayo yajiunge na kampuni binafsi
za bima.
Ameyataja baadhi ya mashirika hayo ya
umma yaliyokaidi kujiunga na NHIF licha ya kulazimishwa kisheria kuwa ni
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti
wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
“Yapo mashirika ya umma yanakataa kujiunga na NHIF wakati sisi
wabunge tumejiunga, wao ni nani? Wakubwa wao wanapata asilimia 10 na wanajiunga
na kampuni za bima ya afya binafsi…
“Mimi niliwahi kuwa Compliance Officer wa NHIF nikaenda TRA,
nikawaeleza umuhimu wa kujiunga NHIF unachangia pesa kidogo unapata huduma
nyingi lakini bosi wao akanijibu pesa si tatizo na afadhali ametumbuliwa huyo
bosi wao, yule angekuwa ofisini kwangu asingetoka,” alisema Mlinga na kuongeza:
“Kila sehemu wananitaja Mlinga Mlinga, napata vitisho vingi
lakini serikali inanilinda na kama jeshi (JWTZ) limeweza kusambaratisha M23
itashindwa kunilinda mimi…wengine wananiita teja hivi teja anavaa suti
iliyonyooka kama mimi, siwezi kukasirika kwa sababu si kweli lakini wangeniita
mbilikimo ningekasirika kwa sababu kweli.”
Mbunge huyo alitaka serikali ikomeshe
tabia ya wanaume kubaka wazee na kufafanua “najiuliza wanawake wa mikoa yenye ubakaji wa
wazee ni wagumu kuelewa hadi wazee wabakwe?”
Naye Mbunge wa Gairo,Mhe. Ahmed Shabiby (CCM) amesema sasa
ataanza kuacha kuwashawishi wananchi wake kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii
(CHF) kutokana na mfuko huo kutopeleka dawa na chanjo za watoto kwenye vituo
vya afya, badala yake inapeleka kondomu na vifaa visivyo muhimu kwa wananchi.SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA.
|
Thursday, May 12, 2016
Home
SIASA
KUTOKA BUNGENI DODOMA:-Mbunge wa Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) Atoa Tuhuma nzito kwa TRA, TCRA, EWURA .
KUTOKA BUNGENI DODOMA:-Mbunge wa Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) Atoa Tuhuma nzito kwa TRA, TCRA, EWURA .
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment