Waliouawa, 1. Feruz
Ismail Elias mika 27, muha imamu wa
msikiti huo na mkazi wa Ibanda relini, 2. Mbwana Rajab miaka 40, mbondei
mfanyabiashara na mkazi wa Ibanda, 3. Khamisi Mponda miaka 28 dereva wa kiwanda
cha samaki (TFP), mkazi wa mkolani, wote walijeruhiwa sehemu za kichwani,
shingoni na mikononi.
Aliyejeruhiwa ni Ismail
Abeid @ ghati miaka 13, mkurya mwanafunzi wa madrasa katika shule ya kiislamu itwayo jabar hila iliyoko
maeneo ya Nyasaka aliyepata majeraha kichwani na anapata matibabu hospitali ya
Nyamagana.
Kutokana na hali hiyo,
waumini wengine walifanikiwa kukimbia huku wakipiga mayowe yaliyopelekea
wahalifu hao kukimbia na kurusha ndani ya msikiti chupa mbili za konyagi
zilizokuwa na petroli na tambi za moto, chupa moja ililipuka lakini haikuleta
madhara makubwa; – Kamanda Ahmed Msangi.
|
Jeshila la polisi limewakamata washukiwa watatu kwa ajili ya
kuwahoji kuhusiana na tukio hilo, huku msako mkali wa kuwasaka watu wengine
walio husika kwa namna moja au nyingine kwenye mauaji hayo ukiwa bado
unaendelea.
Napenda kuwaeleza wananchi watulie wakati tukiendelea na
upelelezi wa tukio hili, na natoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la
polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu wa mauaji hayo ili tuweze kuwakamata.
Pia nashauri na
kusisitiza kuwepo na kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada, kumbi
za starehe pamoja na mitaa yao. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha
ulinzi na usalama katika maeneo hayo.
Imesainiwa na:
……………………….
Sacp: Ahmed Msangi
Kamanda wa Polisi (m)
Mwanza.
|
No comments:
Post a Comment