![]() |
|
Jengo hilo
lililozinduliwa Jana Jumatatu tarehe 09 Mei, 2016 lililopo Jijini Arusha.
|
![]() |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ( PICHANI ) ameyaagiza mashirika yote ya Hifadhi ya jamii
kutoendelea kuwekeza katika miradi ya majengo na badala yake yajielekeze katika
ujenzi wa viwanda na miradi mingine inayozalisha ajira na kuchangia zaidi
katika pato Ia taifa.
Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo Jana Jumatatu tarehe 09 Mei, 2016 alipofungua majengo mawill ya vitega uchumi ya
Mfuko wa Pensheni (PPF) na Shirika Ia Hifadhi ya Jamii(NSSF) yaliyopo Jijini
Arusha.
Pamoja na kuyapongeza mashirika hayo
kwa kujenga majengo ya kisasa jijini Arusha na maeneo mengine hapa nchini, Dkt.
Magufuli amekosoa uwekezaji mkubwa unaofanywa na mashirika hayo kwa kujenga
majengo ya gharama kubwa ambayo licha ya kuwa wananchi wa kawaida hawawezi
kumudu gharama za kupanga kwa ajlli ya kuendesha shughull zao, hayana manufaa
ya kutosha ikilinganishwa na endapo mashirika hayo yangewekeza katika miradi
inayozalisha ajira nyingi, faida ya haraka na kuchangia kwa kiasi kikubwa
katika palo Ia taifa.
|
![]() |
|
Sehemu ya
wadau kutoka NSSF waliohudhuria uzinduzi huo wa wenzao wa PPF.
"Hii mifuko ya hifadhi ya jamii kuanzia leo muache kuwekeza
katika majengo, wekezeni kwenye viwanda, leo mngekuwa na viwanda vya sukari
hawa watu wasingetuchezea kuficha sukari, na inawezekana hata kama ingepungua
tungewambia nyinyi agizeni sukari.
"Mchango wa mifuko ya hifadhi za jamii katika nchi yetu,
ambayo iko saba, imekuwa ikichangia pato la taifa kwa asilimia 12, lakini hifadhi
ya jamii sehemu nyingine duniani, imekuwa ikichangia palo la taifa kwa asilimia
40, kwa hiyo kuna mahali tumekosea, na ndio maana mlipokuwa mkizungumza hapa
sijui mlijua nitakayowaambia, ninawapongeza mliwekeza katika
majengo, jengo Ia PPF na jengo IB NSSF ukipiga hesabu za kawaida haya majengo
yamegharimu zaidi ya shilingi bllioni 60, lakini tujiulize hawa wananchl
waliosimama hapa watayatumiaje haya majengo" Amesema Dk. Magufuli huku akishangiliwa na
wananchi wa Arusha waliojtokeza kushuhudia ufunguzi huo.
|











No comments:
Post a Comment