|
Simba SC imefungwa Bao 1-0 na Mwadui
FC huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kuupeleka Ubingwa wa Msimu huu
kwa Yanga ambao Leo,May 08,2016 hawakucheza na ambao wana Mechi 3 mkononi.
Bao ambalo liliiua Simba SC lilifungwa
Dakika ya 73 na Jamal Nyate katika Mechi ambayo kwenye Dakika za Majeruhi
Mchezaji wa Simba Ajib alitolewa kwa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya.
Simba SC ndio ilikuwa Timu pekee
ambayo ingeweza kuikamata Yanga SC lakini kipigo chao cha Leo kimewaacha na
Pointi 58 na hata wakishinda Mechi zao zote 3 zilizobaki hawawezi kuwafikia
Yanga wenye Pointi 68.
Nako huko Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga, Azam FC walitoka nyuma 1-0 kwa Bao la Dakika ya 24 la Adam Kingwande
na kuichapa Kagera Sugar kwa Bao za Kipindi cha Pili za Kipre Tchetche na Himid
Mao za Dakika za 46 na 59 ambazo ziliwapa ushindi wa 2-1.
Azam FC sasa wamekamata Nafasi ya
Pili wakiwa na Pointi 60 na wamebakisha Mechi 2.
LIGI KUU VODACOM
Msimamo – Timu za Juu:
1 Yanga Mechi 27 Pointi 68
2 Azam FC Mechi 28 Pointi 60
3 Simba Mechi 27 Pointi 58
LIGI KUU VODACOM
RATIBA:
Jumanne Mei 10
Mbeya City v Yanga
Jumatano Me 11
Majimaji v Simba
Jumamosi Mei 14
Mgambo JKT v JKT Ruvu
Ndanda FC v Yanga
Jumapili Mei 15
Mtibwa Sugar v Simba
Kagera Sugar v Stand United
Mwadui FC v Mbeya City
|
No comments:
Post a Comment