Kwenye uwanja wa Azam Complex, Mgambo imeshuka daraja kwa kulazimisha
sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam
FC.
Ramadhani Singano
‘Messi’ alianza kuifungia Azam FC dakika ya 60 kabla ya Fully Maganga kuisawazishaia Mgambo
dakika ya 72.
Mgambo iliyokuwa ikihitaji ushindi kwenye mchezo wa leo imejikuta ikishindwa
kupata ushindi kwa mara nyingine mbele ya Azam
FC ambao sare hiyo imewafanya wamalize kwenye nafasi ya pili nyuma ya
mabingwa Yanga SC.
|
Simba SC waliokuwa wakiwania nafasi ya pili wamechapwa 2 – 1 na Ruvu JKT na timu hiyo iliyo chini ya
kocha wa zamani wa Simba King Kibadeni imenusurika kushuka daraja ,mabao yake
yakifungwa na Abdulrahman Mussa
dakika ya kwanza na 30, wakati la Wekundu wa Msimbazi limefungwa na Nahodha Mussa Hassan Mgosi dakika ya 70.
Kwa matokeo hayo, Azam FC inamaliza na pointi 64,
ikifuatiwa na Simba SC inayomaliza
na pointi 62 katika nafasi ya tatu.
Yanga SC ambayo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu wiki mbili zilizopita, leo,May 22,
2016 imemaliza kwa sare ya kufungana mabao 2 - 2 na wenyeji Majimaji hivyo kufikisha pointi 73.
Mechi nyingine za kufunga pazia la
Ligi Kuu, wenyeji Toto Africans
wamefungwa 1 - 0 na Stand United
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Coastal
Union wamefungwa 2 - 0 na Prisons
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Mbeya City
imelazimishwa sare ya 0 - 0 na Ndanda FC,
Mtibwa Sugar wameichapa 2 - 0 African Sport.
|
Kwa matokeo hayo, timu zote za Tanga,
Mgambo JKT, African Sports na Coastal Union zinaipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu, zikizipisha Ruvu Shooting, Mbao FC na African Lyon.
Mgambo JKT imemaliza na pointi 28, African
Sports pinti 26 na Coastal Union pointi 22.
|
No comments:
Post a Comment