MAKAMU WA RAIS TANZANIA:-Aagiza Wakuu wa Mikoa ya Geita, Arusha na Kagera Kuondoa Mifugo na Wanachi waliovamia maeneo ya hifadhi za taifa ifikapo Juni 30,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 17, 2016

MAKAMU WA RAIS TANZANIA:-Aagiza Wakuu wa Mikoa ya Geita, Arusha na Kagera Kuondoa Mifugo na Wanachi waliovamia maeneo ya hifadhi za taifa ifikapo Juni 30,2016.

Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Samia Hassan Suluhu akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na Mameneja wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kukabidhi hundi kwa wakuu wa mikoa 19 inayopakana na Hifadhi za Taifa ambazo wilaya zake zimepata msaada huo wenye thamani ya kiasi cha Sh, Bilioni moja.

Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan ameagiza Wakuu wa mikoa ya Geita, Arusha na Kagera kuhakikisha wanaondoa mifugo itokayo nje ya nchi pamoja na kuwaondoa wanachi waliovamia maeneo ya hifadhi za taifa (TANAPA) ifikapo Juni 30 mwaka huu,2016.

Aidha ameagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanatenga maeneo maalumu kwa ajili ya mifugo inayotolewa ndani ya hifadhi na kupunguza mgogoro kwa wananchi wengine.

Mhe.Samia alitoa maagizo hayo jana,May 16,2016, wakati alipokuwa akikabidhi hundi ya thamani ya Sh bilioni moja kwa wakuu wa mikoa 19 inayozunguka hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kununua madawati. Alisema, wakuu wa mikoa wakizembea kutekeleza uondoaji mifugo ndani ya hifadhi za taifa serikali itawawajibisha.
Alisema waliohifadhi mifugo ndani ya hifadhi hiyo waondoke na mifugo yao hadi Juni 30 mwaka huu kwani mkoa wa Kagera una ng’ombe milioni mbili wanaotoka nje ya nchi, na mikoa ya Arusha na Geita ina ng’ombe milioni tatu kutoka nje ya nchi.

Akizungumzia kuhusu kukabidhi madawati 16,500 katika wilaya zote 55 zilizopo kwenye mikoa 19 nchini, Mhe.Samia aliipongeza TANAPA kwa kusaidia Elimu nchini kwani baada ya serikali ilipotangaza kuwa elimu bure wanafunzi wengi wamejitokeza huku kukiwa na changamoto ya madawati,Mhe. Samia alisema, kutokana na msaada huo wanafunzi wataondokana na adha ya kukaa chini na kuumia migongo kwani kila wilaya itapata madawati 300 huku wanafunzi 49,500 wakiwa wanakaa kwenye madawati na kuongeza usikivu zaidi.
Baaadhi ya wakuu wa wilaya waliowakilisha wakuu wa mikoa yao katika hafa fupi ya utoaji wa Hundi kwa ajili ya Madawati katika wilaya 55 zinazopakana na Hifadhi za Taifa.
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema Tanapa wanatambua mchango wa elimu ndio maana wametoa msaada huo kwa mikoa 19 inayopakana na hifadhi za taifa.

Baadhi ya Wakurugenzi na watendaji wengine wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Saidi Mecky Sadicky akitoa neno la shkurani kwa niaba ya wakuu wengine wa mikoa kwa msaada huo wa pesa kwa ajili ya Madawati ,kiasi cha Sh Bilioni moja kilichotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Mkurugenzi wa Tanapa, Allan Kijazi alisema Tanapa itaendelea kushirikiana na serikali katika sekta ya elimu kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa bidii pamoja na kujua jinsi ya kuhifadhi maliasili za Taifa.


Akitoa salamu za shukrani kwa Makamu wa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki aliishukuru Tanapa kwa kutoa madawati kwa wakuu wa mikoa na kusema kuwa, mkoa wa Kilimanjaro umepiga marufuku usafirishaji wanyama pori kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuanzia jana,May 16, 2016.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za taifa nchini (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa utaratibu wa namna wakuu wa mikoa atakavyopokea Hundi kutoka kwa Makamu wa Raisi ,Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongera ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa mkoa wa Tanga ,Martin Shigela ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa. 

Wengine kulia mwa Makamu wa Rais ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini Allan Kijazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa mkoa wa Katavi ,Meja Jenerali Mstaafu ,Raphael Muhuga ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa wilaya ya Mvomero ,Betty Mkwasa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa wilaya ya Tarime,Glorious Luoga kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mara ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa. 

Wengine kulia mwa Makamu wa Rais ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini Allan Kijazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Hassan Suluhu akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa ,Kamishna wa Polisi Mstaafu,Zelothe Stephen ikiwa ni mchango wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya ununuzi wa Madawati katika shule zilizopo katika wilaya zinazipakana na Hifadhi za Taifa. 

Wengine kulia mwa Makamu wa Rais ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini Allan Kijazi. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad