Magari ya
washawasha Jana,May 11,2016, yaliibua mjadala bungeni baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe.Susan Lyimo (CHADEMA)
kubanwa athibitishe kauli yake aliyoitoa
kuwa serikali ilinunua magari ya Polisi ‘Washawasha” 777 wakati ilitumia
50 pekee wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.
Mbunge huyo
alitakiwa kuthibitisha hilo na Mwenyekiti wa Bunge, Mhe.Mussa Azzan Zungu kwa
kupeleka uthibitisho au kufuta kauli yake baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Yussuf Massauni kuomba mwongozo kupitia kanuni ya 64(a) na
63(1) akiomba mwongozo wa hatua gani anaweza kuchukuliwa Lyimo.
“Kanuni
zipo, zinampa haki kila mbunge na Naibu Waziri ameomba mwongozo kwa kanuni ya
64(a) na 63(1) sasa kwa kuwa Susan hayupo hapa sasa hivi, akirejea jioni
mwongozo wangu ni kwamba afute maneno yake au alete uthibitisho,” alisema Mwenyekiti
huyo wa Bunge.
Mhe.Lyimo katika
mchango wake kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
alisema serikali imenunua magari ya ‘Washawasha” 777 mwaka jana wakati wa
Uchaguzi Mkuu lakini yaliyotumika ni 50 pekee.
|
No comments:
Post a Comment