Wawakilishi
wa Simon Msuva wakipokea tuzo ya mchezaji bora wa VPL msimu uliopita
iliyonyakuliwa na nyota huyo wa Yanga SC kwenye sherehe za ugawaji tuzo za VPL
msimu uliopita (2014-2015).
Na Baraka
Mbolembolea
Ligi Kuu ya
Soka Tanzania Bara (VPL) 2015/2016 itafikia mwisho wikendi ijayo kwa timu zote 16
kucheza game zao za 30.
Mechi nane zitapigwa wikendi hii ili kukamilisha
mzunguko wa 29. Jumamosi May 14,2016,itachezwa michezo miwili (JKT Mgambo v JKT Ruvu na
Ndanda SC v Yanga SC).
Tayari Bingwa wa msimu huu amekwisha fahamika ( Yanga SC ) ambao watakabidhiwa kombe lao May 14,2016 na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Mhe Mwigulu Nchemba.
Hapa nakuletea thamani ya zawadi mbalimbali ambazo wadhamini wakuu
wa ligi hiyo kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom watazitoa kwa washindi.
BINGWA
KULAMBA TSH. 81 MIL
Yanga
SC itaingiza zaidi ya milioni 81 katika akaunti yao kutokana na kutwaa kwao taji
hilo.
MSHINDI WA
PILI
Mshindi wa
pili katika ligi hiyo anataraji kuvuna kiasi cha milioni 40. Nafasi hii hadi
sasa inawaniwa na timu za Azam FC na Simba SC.
MSHINDI WA
TATU
Timu
itakayomaliza nafasi ya tatu yenyewe itafanikiwa kujipatia kiasi cha milion 29.
MSHINDI WA
NNE
Mtibwa Sugar
ikiwa itamaliza katika nafasi ya nne waliyopo kabla ya game mbili za mwisho
inaweza kupata milioni 23 kama zawadi ya mshindi wa nafasi hiyo.
MFUNGAJI
BORA
Mrundi, Amis
Tambwe anasaka tuzo yake ya pili ya ufungaji bora katika VPL. Akiwa amekwishafunga
jumla ya magoli 21 hadi sasa, mfungaji huyo bora wa msimu wa 2013/2014 anaweza
kujiingizia kiasi cha milioni 5.4 kama zawadi ya mfungaji bora.
MCHEZAJI
BORA WA LIGI
Mshindi wa
tuzo hii msimu uliopita ni kiungo mshambulizi wa Yanga SC, Saimon Msuva. Unajua
mchezaji bora wa msimu atavuna kiasi gani? Ni kiasi cha milioni 5.4.
GOLIKIPA
BORA
Kama ilivyo
kwa mfungaji bora na mchezaji bora wa msimu, tuzo ya kipa bora pia itaambatana
na zawadi ya milioni 5.4.
TIMU YENYE
NIDHAMU
Klabu yenye
kadi chache na iliyoonyesha uungwana kwa msimu mzima itazawadiwa kiasi cha
milion 17.
KOCHA BORA
Tuzo hii
ilizua maneno mengi msimu uliopita baada ya Mbwana Makatta aliyekuwa
ameisimamia Kagera Sugar kutangazwa mshindi licha ya kwamba alikuwa katika
msimu kwa game nane tu.
Tuzo ya kocha bora itaendana na zawadi ya milioni 8.
MWAMUZI BORA
Mwamuzi
atakayekuwa amefanya vizuri kwa msimu mzima atazawadiwa tuzo na kiasi cha
milioni 8 pesa taslim.
|
No comments:
Post a Comment