RAIS MAGUFULI:-‘’…Shinyanga imefikisha Watumishi Hewa 226 hadi Sasa..’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 19, 2016

RAIS MAGUFULI:-‘’…Shinyanga imefikisha Watumishi Hewa 226 hadi Sasa..’’


Idadi ya wafanyakazi hewa katika mkoa wa Shinyanga ambao kwa mustakabali wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bi. Anne Kilango Malecela kudai kutokua na Watumishi hewa hata mmoja imeongezeka na kufikia 226.

Hayo yamebainishwa leo,April 19,2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli katika uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, ambapo alisisitiza kuwa Serikali yake haitawafumbia macho viongozi ambao kwa namna moja au nyingine wataruhusu mianya ya ubadhirifu wa fedha katika maeneo yao.

''..Mkoa wa Shinyanga kwa taarifa nilizonazo hadi sasa wameshapatikana wafanyakazi hewa 226 kutoka ‘zero’ hivyo ni lazima tuwajibike kwa watanzania wanyonge,” ....alisema Rais Magufuli.


Wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mikoa Serikalini, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anne Kilango Malecela alisema mkoa wake hauna Mtumishi hewa hata mmoja jambo lililopelekea Rais Magufuli kuunda tume iliyobaini watumishi hewa  45 katika awamu ya kwanza.


Baada ya kubainika uwepo wa watumishi hao, Rais alitangaza kutengua Uteuzi wa Mkuu huyo wa Mkoa ( Pichani ) kwa kutokuwa makini na taarifa anazopewa na wasaidizi wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad