![]() |
|
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mwenge wa
Uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka
mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za
Tanzania.Picha na OMR.
|
![]() |
|
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Taifa
kwenye Sherehe za uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa zilizofanyika leo april
18, 2016 katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
|
![]() |
|
Mwenge wa Uhuru umezinduliwa rasmi
mbio zake ili kukimbizwa katika halmashauri za wilaya na Manispaa zipatazo 179
za mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Baada ya kuwashwa leo, Mwenge wa
Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kuhitimishwa
wilayani Gairo ambako Aprili 25, mwaka huu,2016 utakabidhiwa mpakani mwa wilaya
hiyo na Kilindi ya Mkoa wa Tanga ili kuendelea na mbio zake.
Mwenge wa Uhuru uliwashwa kwa mara ya
kwanza Desemba 9, 1961 kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro, kutimiza ahadi ya
Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kudai Uhuru wa
Tanganyika.
|









No comments:
Post a Comment