MATOKEO / RATIBA LA LIGA 2015/2016:-Barcelona Yatumbuliwa Tena.! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 18, 2016

MATOKEO / RATIBA LA LIGA 2015/2016:-Barcelona Yatumbuliwa Tena.!

33476D1F00000578-3544760-image-a-65_14609248178994
Ilikuwa ni mechi ya nne kwa Barcelona kufungwa mfurulizo.

Japo  Lionel Messi kufunga bao lake la 500, Barcelona jana,April 17,2016 ilikubali kichapo kingine cha bao 2-1 kutoka kwa Valencia kwenye Uwanja wa Nou Camp. 

Ni miaka 13 sasa tangu Barcelona wafungwe na Valencia lakini jana hali ilikuwa tofauti.

 Valencia ilipata bao la kwanza dakika ya 26, baada ya Guilherme Siquiera kupiga krosi iliyompalaza Ivan Rakitic na kumfungisha kipa wake.
3347567500000578-3544760-image-a-50_1460923510258
Messi akijaribu kuwatoka mabeki wa Valencia.
3347651100000578-3544760-image-a-67_1460925011726
Santi Mina alionbgeza bao la pili kwa Valencia dakika ya 45 kabla ya kwenda mapumziko.

Lionel Messi aliipa Barcelona Bao lao pekee katika Dakika ya 63 akifuta ukame wa kutofunga katika Mechi 5 na hilo kuwa Goli lake la 500 katika maisha yake ya Soka.

33471AB300000578-0-image-a-10_1460921220115

33471B9C00000578-3544760-image-m-41_1460923475787
Kwa kipigo hicho,kimewaacha Barcelona bado wanaongoza La Liga 2015/2016 wakiwa Pointi sawa na Atletico Madrid  kwa Pointi 76 huku Real Madrid wakiwa na Pointi 75 nyuma yao na hali hii inazidisha uhondo wa La Liga ambayo inaelekea ukingoni zikibakia Mechi 5 kwisha.

Jumatano,April 20,2016 Timu zote hizi 3 zote dimbani kwa Barcelona kucheza na Deportivo La Coruna, Atletico Madrid kuwa Ugenini na Athletic Bilbao wakati Real Madrid wako kwao kucheza na Villareal.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad