MATOKEO / RATIBA EPL 2015/2016:- Leicester City na Hatua ya Ubingwa huku Manchester United hoi White hart Lane. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 10, 2016

MATOKEO / RATIBA EPL 2015/2016:- Leicester City na Hatua ya Ubingwa huku Manchester United hoi White hart Lane.


Mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy akipongezwa na Wachezaji wenzake  baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 66’’ na 90’’katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Sunderland kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza leo hii April 10,2016 Mapema huko Stadium of Light.

Leicester City sasa wamebakisha Mechi 5 kumaliza Ligi na wanahitaji ushindi katika Mechi 3 kati ya hizo ili kubeba Taji bila ya kujali matokeo ya Timu nyingine.
Sunderland, wamebaki Nafasi ya 18 ambayo ndio ya mwisho kushushwa Daraja na wako Pointi 4 nyuma ya Norwich City iliyo Nafasi ya usalama ya 17 lakini afueni kwa Sunderland ni kuwa Norwich wamecheza Mechi 1 zaidi yao na watapambana nao Wikiendi ijayo huko Carrow Road.

Huko Anfield, Liverpool waliitandika Stoke City Bao 4-1 kwa Bao za Alberto Moreno Dakika ya 8, Daniel Sturridge, 32, Divock Origi, 50 na 65 na lile la Stoke City kufungwa na Bojan Krkic katika Dakika ya 22.

Ushindi huu umewaweka Liverpool Nafasi ya 8 wakiwa na Pointi 48 wakati Stoke City wapo Nafasi ya 9 wakiwa na Pointi 47.

Nao Tottenham ndani ya dakika 6 ikapata ushindi wa mabao 3-0  walipoichapa Manchester United nyumabni White Hart Lane Jijini London .

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Tottenham dhidi ya Manchester United tangu 2001 Uwanjani hapo na umewaweka nafasi ya Pili  kwa Pointi 7 nyuma ya Lecester City.

Bao za Spurs zilifungwa Dakika za 70, 74 na 76 kupitia Dele Alli, Toby Alderweireld na Erik Lamela.

Kipigo hiki kimewaacha Manchester United Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 4 Manchester City na kuyafanya matumaini yao kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE  Msimu ujao kufifia na pia kulianzisha upya sakata la Mashabiki kumtaka Meneja Louis van Gaal ang’oke.

Ratiba:

Jumatano Aprili 13,2016.

2200 Crystal Palace v Everton    

Jumamosi Aprili 16,2016.

1445 Norwich v Sunderland                 

1700 Everton v Southampton               

1700 Man Utd v Aston Villa         

1700 Newcastle v Swansea         

1700 West Brom v Watford         

1930 Chelsea v Man City  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad