MAHAFALI KIDATO CHA SITA KABANGA SEKONDARI NGARA:-Tazama Taswira Yake Jana April 16, 2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 17, 2016

MAHAFALI KIDATO CHA SITA KABANGA SEKONDARI NGARA:-Tazama Taswira Yake Jana April 16, 2016.

Pichani wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ,Dkt.Elia Kibwa akikata utepe kufungua Mahafali ya 6 ya Kidato cha Sita 2016 ya Shule ya Sekondari Kabanga ,wilayani Ngara mkoani Kagera jana April 16, 2016.

Kulia  ni Mkuu wa Shule hiyo Bw Aaron Dishon Sekazoya,na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Bw.Julius Sendama na Kaimu Afisa Elimu Idara ya Sekondari wilayani Ngara Bw Gerald Muhile (kushoto.)

Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari kabanga wilayani Ngara Mkoani Kagera, wameitaka serikali   kuboresha elimu nchini kwa kweka miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika shule za msingi sekondari 

Wamebainisha hayo jana April 16, 2016, katika mahafali  ya sita ya shule hiyo kwa kidato cha sita na kwamba katika shule nyingi hapa nchini zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa , matundu ya vyoo, madawati, vitabu vya kiada na ziada pamoja na uhaba wa maktaba zenye viwango katika utoaji wa taaluma ya elimu.

Wahitimu hao 147 wa kidato cha sita kati yao wasichana ni 46 na wavulana ni 101 walio katika mchepuo wa masomo ya CBG na HKL huku  shule yote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha tano jumla yao ni wanafunzi 869 kati yao  wasichana ni 388.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kabanga ,Bw. Aaron Dishon Sekazoya akitoa taarifa ya Maendeleo na Changamoto mbalimbali katika Shule yake wakati wa Mahafali ya 6 ya Kidato cha Sita 2016 Shule ya Sekondari Kabanga ,wilayani Ngara mkoani Kagera jana April 16, 2016.

Wanafunzi wa shule hiyo  wamesema wanakabiliwa na changamoto ya malazi kwa kukosa mabweni kwani wanatumia vyumba vya madarasa na kulala wanafunzi wawili katika kitanda kimoja kwa kuwa vitanda ni pungufu

Licha ya kupata chakula  hapa shuleni tunapanga foleni kutafuta huduma ya choo na wengine tunachafua mazingira tukijisaidia vichakani  jambo ambalo tunahofia kukumbwa na magonjwa ya mlipuko” Alisema mmoja wa Wanafunzi wa shule hiyo.

Aidha  shule hiyo haina bwalo  na wanafunzi kulia chakula chini ya miti huku wakikosa maktaba, vitabu vya masomo ya Sayansi, walimu wa masomo hayo pamoja na kukatika kwa umeme na maji na  kuwakatisha tamaa katika taaluma.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ,Dkt.Elia Kibwa akikabidhi Cheti kwa mmoja wa Mhitimu wa Kidato cha Sita wakati wa  Mahafali ya 6 ya Kidato cha Sita 2016 ya Shule ya Sekondari Kabanga ,wilayani Ngara mkoani Kagera jana April 16, 2016.
Mkuu wa shule hiyo Bw.Aaron Dishon Sekazoya ( Pichani ) amesema jitihada zilizofanywa na shule hiyo ni kukarabati madawati 150 na vitanda 46 kwa thamani ya Sh150 000 na kwamba kanisa la Anglikan wilayani Ngara kupitiaTumaini Fund utajenga matundu 10 ya vyoo kwa thamani ya Sh40 milioni.

Bw.Sekazoya amesema changamoto zilizotajwa  za kukosa bwalo na ukumbi wa mikutano ni pamoja na uhaba wa Hostel, kwani iliyopo ni moja yenye kutosheleza wanafunzi 90 tu na mabweni yapo mawili na kuhitajika mabweni matatu.

Amesema shule hiyo inahitaji vitanda 200 vya wanafunzi vilivyopo  174 vinavyotumiwa na  wanafunzi 87 walioko katika hostel tatu  nab ado mahitaji ni nyingine tatu zenye kutumiwa na wanafunzi 240

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dr Elia Kibwa ambaye ni mkazi wa wilaya ya Ngara ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo  , amesema   walimu waandae mazingira ya wanafunzi kwa kupanda miti ambayo itawasaidia kupata zana za kufundishia

Aidha amesema akiwa ndiye mwalimu wa kwanza katika shule hiyo mwaka 1990  ndoto  zake ni   wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi sita   kujengwa kisaikolojia kuingia katika Chuo Kikuu  kwa kuwa na ujuzi   kupitia masomo ya Sayansi.

Ndoto zangu nahitaji watakaomaliza kidato cha sita hapa waingie Chuo kikuu katika  wilaya yetu ili wazawa  wapate wageni kutoka wilaya na mikoa mingine na kujifunza mila na tamaduni za makabila mbalimbali” Alisema Dr Elia Kibwa.

Katika hatua nyingine amesisitiza walimu kuwafundisha wanafunzi masomo ya Sayansi , Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA ili kuingia katika ushindani wa kimawasiliano katika kujifunza wakitumia mitandao na kompyuta

HABARI/PICHA Na:-Shaaban Ndyamukama-Ngara/Kagera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad