MATOKEO / RATIBA VPL 2015/2016:-Simba SC Yashindwa kuwashusha Yanga SC kileleni wakifungwa 1 – 0 Leo April 17, 2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 17, 2016

MATOKEO / RATIBA VPL 2015/2016:-Simba SC Yashindwa kuwashusha Yanga SC kileleni wakifungwa 1 – 0 Leo April 17, 2016.


Timu ya 'Wekundu wa Msimbazi' Simba SC,wamepata pigo katika harakati za kuutafuta Ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu 2015/2016 baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 toka kwa Toto African ya Mwanza kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,Jioni ya leo April 17, 2016.


Toto African ambao walikuwa wakifanya mashambulizi ya kushtukiza na kutumia mipira mirefu walifanikiwa kupata goli la kuongoza dakika ya 21 kupitia kwa Waziri Junior aliyepiga shuti kali lililomshinda golikipa Vicent Agban na kutinga wavuni.

Waziri aliutumia vema mpira mrefu uliogongwa kichwa na Edward Christopher na kumkuta yeye akiwa kwenye nafasi nzuri.



Dakika ya 30 Kocha wa Simba SC,Jackson Mayanja alitolewa nje na mwamuzi Ahmed Simba toka Kagera baada ya kutoa lugha isiyofaa kutokana na mchezaji wake kufanyiwa madhambi na mchezaji wa Toto African.



Pia Dakika moja baada ya kuanza kipindi cha pili beki Hassani Kessy alioneshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Edward Christopher.



Kwa matokeo hayo sasa,Simba SC wamebakia na pointi zao 57 na kuendelea kushika nafasi ya pili baada ya kushindwa kuwashusha Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo,Yanga SC kileleni wakiwa na alama 59.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad