AJALI / PICHA:-Tundaman anusurika kifo ajalini Leo April 17,2016 huku aliyekuwa akiendesha apoteza Maisha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 17, 2016

AJALI / PICHA:-Tundaman anusurika kifo ajalini Leo April 17,2016 huku aliyekuwa akiendesha apoteza Maisha.

Taswira za ajali aliyoipata Tundaman leo April 17,2016.

Mwanamuziki wa Muziki wa Kizazi Kipya, Tunda Man leo,Jumapili April 17,2016, amenusirika kifo baada ya kupata ajali mbaya eneo la Idetelo, katikati ya Nyololo la Makambako.

Kwa mujibu wa Tunda Man  akiwa amesinzia ghafla alisikia mlio mkubwa uliopelekea gari yao kupoteza muelekeo na kuelekea porini, ndani ya gari yao kulikuwana watu watano ambao mmoja wao alifariki dunia papo hapo huku wengine wakijeruhiwa.

Aidha Tunda Man amemtaja marehemu kuwa ni  Mussa maarufu kwa jina la Man Katuzo ambaye taratibu za kusafirisha mwili wake kuupeleka Kilosa mkoni Morogoro zinaendelea.
Tundaman akiwa na marehemu Mussa maarufu kwa jina la Man Katuzo enzi za uhai wake.


Taswira za ajali aliyoipata Tundaman leo April 17,2016.
Tundaman (kushoto) akiwa na Stamina (katikati) pamoja na marehemu Man Katuzo enzi za uhai wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad