KOMBE LA SHIRIKISHO:-April 24,2016 Coastal Union na Yanga SC – Mwadui FC na Azam FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 13, 2016

KOMBE LA SHIRIKISHO:-April 24,2016 Coastal Union na Yanga SC – Mwadui FC na Azam FC.

Droo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) imefanyika Jana April 12, 2016,Usiku.

Katika droo hiyo iliyochezeshwa na mchezaji mstaafu wa timu ya timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars), Esther Chaburuma, imewashuhudia vigogo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Azam FC na Yanga SC wakipata nafasi ya kucheza michezo hiyo katika viwanja vya ugenini.

 Mwadui FC watakua wenyeji wa Azam FC katika mchezo unaotarajiwa kucheza Aprili 24, 2016 mjini Shinyanga, huku wagosi wa Kaya Coastal Union wakicheza dhidi ya Yanga SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga siku hiyo hiyo.

Washindi wa michezo hiyo ya Nusu Fainali, watakutana fainali ya kombe hilo itakayofanyika mwezi Mei, ambapo Bingwa wake ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC).
AdTech AdAdTech Ad

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad