KLABU BINGWA ULAYA:-Real Madrid na Manchester City zaenda Nusu Fainali Leo April 13,Barcelona na Bayern Munich Kufuzu..??? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 13, 2016

KLABU BINGWA ULAYA:-Real Madrid na Manchester City zaenda Nusu Fainali Leo April 13,Barcelona na Bayern Munich Kufuzu..???

Kutana natakwimu za Ronaldo na Madrid ndani ya UEFA Champions League.

Ronaldo amefunga magoli 34 (na ana-assist nane) kwenye mechi 36 za Champions League hatua ya mtoano akiwa Real Madrid.

Ronaldo amefunga magoli 62 kwenye mechi tofauti za Champions League; zaidi ya mchezaji yeyote (anafuatiwa na Raul mwenye magoli 56)

Nyota huyo wa Ureno amesha kwamisha mpira nyavuni mara 16 kwenye mashindano ya Champions League msimu huu.

Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kati ya mara 16 timu kupoteza mchezo wa ugenini kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Champions League kisha kusonga mbele baada ya mchezo wa marudiano (Barcelona vs AC Milan 2013 na Man United vs Olympiacos 2014)

Madrid ndiyo timu pekee ambayo haijaruhusu kufungwa bao kwenye uwanja wake wa nyumani kwenye michuano ya Champions League msimu huu.


Real Madrid na Manchester City zimekuwa Timu za kwanza kutinga Nusu Fainali baada ya kushinda Mechi zao za Marudiano ya Robo Fainali ya UEFA Champions League 2015/2016.

Leo Jumatano,April 13, 2016, Usiku Mechi za Robo Fainali zitakamilika kupata Washindi wawili wengine na Ijumaa itafanyika Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali.

Atletico Madrid wakiikaribisha FC Barcelona, zote za Hispania Uwanja wa Vicente Calderon na Benfica ya Ureno wakiwa wenyeji wa Bayern Munich Kwenye Uwanja wa Luz.

Mechi za kwanza wiki iliyopita, Bayern ilishinda 1-0 na Barcelona ilishinda 2-1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad