


![]() |
|
Akizungumzia
baada ya misa hiyo Rais Magufuli amesema anamkumbuka Hayati Edward Moringe
Sokoine, kuwa alikuwa kiongozi shupavu aliyewapenda watanzania, aliyependa
kuwatumikia watanzania, aliyekuwa Mchapakazi, aliyechukia rushwa, aliyechukia
ufisadi na aliyechukia uonevu kwa watu wa chini.
"Namuona ni kilelezo cha pekee katika
Taifa letu la Tanzania, miaka 32 iliyopita wakati Mzee wetu Hayati Edward
Moringe Sokine alipoitwa na kutangulia mbele za haki, wakati huo mimi nilikuwa
JKT Mpwapwa, ninaikumbuka siku hiyo ilikuwa ya majonzi makubwa" Amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo
Rais Magufuli amesema kazi nzuri ya mtu huwa haipotei na hivyo amewasihi
watanzania kuendelea kushikamana, kupendana na kuyaenzi mazuri yote
yaliyofanywa na viongozi wa Taifa waliotangulia mbele za haki, wakiwemo hayati
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Hayati Abeid Amani Karume na
Hayati Edward Moringe Sokoine.
|
![]() |
|
Kwa upande
wake Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa
amemuelezea Hayati Sokoine kuwa ni Kiongozi aliyejitoa kutumikia Taifa, na
kubainisha kuwa viongozi wote wanawajibika kuishi kwa mfano wake.
Rais Mstaafu
Mkapa amesisitiza kuwa mfano huo wa Hayati Sokoine, ndio ulioiwezesha Tanzania
kumpata kiongozi wa Sasa, Rais John Pombe Magufuli anayetaka kuonesha misingi
ya uongozi bora, uadilifu, kusimamia amani, utulivu na maendeleo.
Nae Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
amesema Hayati Sokoine hakuwa kiongozi wa kujiangalia yeye, bali Kiongozi kwa
ajili ya watu, na amempongeza Rais Magufuli kwa kufuata nyayo za Hayati Sokoine
katika kuliongoza Taifa.
"Kuna
baadhi ya watu wanasema Rais wetu wa sasa ni sura ya Edward Moringe
Sokoine" Amesema Kardinali Pengo, na kumtaka Rais Magufuli na serikali
yake kusonga mbele na kujenga heshima ya nchi.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
12 Aprili,
2016
|








No comments:
Post a Comment