![]() |
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe
Magufuli amesema amewatuma watu kuwarekodi mawaziri ambao wamesikika
wakilalamika 'chinichini' kukatwa kwa fedha za matumizi mengineyo ( OC- Other
Charges ) katika bajeti ya serikali ya
mwaka ujao wa fedha.
"Mawaziri
wengine nasikia wanalalamika kweli,sasa nimetuma watu kuwarekodi kwa sababu
mind set (fikra) zao bado hazijabadilika,wanafikiri watu bado tupo kwenye
trend hiyo hiyo,wasomi ni wengi,unaweza
ukawateua leo na kesho ukawabadilisha, ili mradi twende kwenye trend
ninayoitaka," alisema Magufuli.
Rais
Magufuli aliyasema hayo jana,aPRIL 11,2016, Ikulu
jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia hatua ya bunge kubana matumizi na
kuwezesha kupatikana kwa kiasi cha shilingi bilioni 6 ambazo zitaelekezwa
kwenye utengenezaji wa madawati.
“Chief
Secretary(Katibu Mkuu Kiongozi ), huo ndio muelekeo kwa Makatibu Wakuu, waache
kudai OC… Nawasikia watu wanadai eti OC ni kidogo. Wakiona hazitoshi basi
waache kazi, maana wenzao wabunge wamesema ni nyingi na wamebana
matumizi," alisema Rais Magufuli na kuongeza:
"Katibu
wa bunge ameonyesha mfano,kwa nini wengine washindwe? Mtaona katika bajeti
tumekata hizo OC ambazo zilikuwa ni ulaji mtupu, tumeongeza bajeti ya maendeleo
kutoka kati ya bilioni 26 na 27 hivi za mwaka jana hadi asilimia 40, fedha za
bajeti ziende kufanya miradi ya maendeleo, zikawasaidie watu masikini."BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
|
Tuesday, April 12, 2016
Home
HABARI
SIASA
HAPA KAZI TU:-Rais Magufuli Asema Ametuma Watu Kuwarekodi Mawaziri Wanaolalamika ili nao Awatumbue Majipu.
HAPA KAZI TU:-Rais Magufuli Asema Ametuma Watu Kuwarekodi Mawaziri Wanaolalamika ili nao Awatumbue Majipu.
Tags
# HABARI
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment