Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ameweka jiwe la msingi kwa ajili
ya kuanza rasmi ujenzi wa barabara ya
juu kwenye makutano ya barabara za Nyerere na Mandela eneo la Tazara jijini Dar
es Salaam leo.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Rais Magufuli amesema ujenzi huo wa barabara ya juu
utaanza mara moja kwa ushirikiano na serikali ya Japan na utagharimu Shilingi 100 bilioni.
Amesema,
serikali ya Japan imefadhili mradi huo kwa Sh 93.44 bilioni wakati serikali ya
Tanzania imechangia Sh 8.36 bilioni na unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba
2018.





No comments:
Post a Comment