ZIARA YA SIKU 14 KANDA YA ZIWA:-Waziri Mkuu atatembelea mikoa ya Simiyu, Kigoma, Geita na Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 02, 2016

ZIARA YA SIKU 14 KANDA YA ZIWA:-Waziri Mkuu atatembelea mikoa ya Simiyu, Kigoma, Geita na Kagera.

Waziri Mkuu wa Tanzania,Bw. Kassim Majaliwa akiwasalimu wananchi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 01, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw.Magesa Mulongo.

Waziri Mkuu,Bw Kassimu Majaliwa hapo Jana Machi 01, 2016, amewasili Jijini Mwanza kuanza ziara ya siku 14 katika mikoa ya Kanda Ziwa kukagua shughuli na miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw.Magesa Mulongo amesema Waziri Mkuu atatembelea mikoa ya Simiyu, Kigoma, Geita na Kagera.
 
Wakati huohuo; Bw.Mulongo amesema mke wa Rais, Janet Magufuli anatarajiwa kutembelea Kituo cha Kulea Wazee Bukumbi kilichopo wilayani Misungwi.

Ziara hii ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8, kila mwaka,” alisema Mulongo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi, Angelina Mabulla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 01, 2016.
Waziri Mkuu wa Tanzania,Bw. Kassim Majliwa akitazama ngoma  ya nyoka baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo,Bw. Magessa Mulongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad