Rais wa
Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye koti la
drafti) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, Leo 09 Machi, 2016
kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati
ya Tanzania na Vietnam.
Kulia niRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
John Pombe Joseph Magufuli.
|
Rais wa
Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa tatu
kushoto) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam ,Leo 09 Machi,
2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali
kati ya Tanzania na Vietnam.
Wa pili kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili
kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakipanda
jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride , Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) pamoja
na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakiwa katika jukwaa kwa
ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa .
|
Rais wa
Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (mwenye tai nyekundu) akikagua gwaride la heshima
katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam ,Leo 09 Machi, 2016.
|
Mke wa Rais
wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akipokea zawadi ya ua toka kwa mtoto mara
alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam , Leo 09 Machi, 2016 akiwa
amefuatana na mmewe kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika
nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.
|
Rais wa
Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe mama Mai Thi Hanh
wakiwasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, Leo 09 Machi, 2016 kwa ajili
ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbalikati ya Tanzania
na Vietnam.
(Picha Zote Na Benedict Liwenga-MAELEZO).
|
No comments:
Post a Comment