|
Huku kukiwa
na taarifa kuwa wasaliti wa CCM wanaotarajiwa kutimuliwa wengi ni watu maarufu
hasa viongozi wa ngazi za mkoa, tayari viongozi 21 wa Manyara, wameshatumbuliwa
majipu bila ganzi.
Jumla ya
viongozi 21, watatu wakiwa ni wa CCM Wilaya ya Babati Mjini mkoani Manyara na
wengine 18 wa ngazi ya kata, wameshaadhibiwa na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya
Kikwete alichokiita kutumbua majipu bila aibu.
Inadaiwa
kuwa viongozi hao walikuwa wanamshabikia aliyekuwa mgombea urais wa Chadema,
Edward Lowassa.
Imedaiwa
ushabiki ulisababisha CCM ipoteze jimbo na kata tano kati ya nane za Babati
Mjini.
Katibu wa
CCM mkoani Manyara, Ndeng’aso Ndekubali aliwataja waliofukuzwa uanachama kuwa
ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, Cosmas Masauda, Zulekha Mohamed na
mjumbe wa mkoa, Felix Kivuyo.
“Hawa
wamefutwa uanachama baada ya kudaiwa kukisaliti chama kwa kuwapigia kampeni
wagombea wa vyama vya upinzani na kuwaombea kura kwenye Uchaguzi Mkuu,” alidai
Ndekubali.
Februari 24,
mwaka huu, Kikwete alipokuwa akizindua nyumba ya chama hicho Kibaha mkoani
Pwani, alisema mwanachama yeyote aliyekihujumu chama chao kwenye uchaguzi wa
mwaka jana, atatumbuliwa jipu bila aibu.
Kikwete
alikaririwa akisema tayari CCM ina majina ya wasaliti wote na mchakato wa
kuwaadhibu unaendelea kuanzia ngazi ya matawi, kata, wilaya mkoa na Taifa.
Alisema viongozi hao wamekiuka ibara ya 93, kifungu cha 14 ya Katiba ya CCM.
“Halmashauri
Kuu ya CCM mkoa, imewavua nyadhifa viongozi 18 wa ngazi za kata wilayani Babati
Mjini kwa kukiuka maadili, kushiriki ubadhirifu wa fedha na kukosa uaminifu,”
alisema Ndekubali.
Alisema
viongozi 18 wa ngazi ya kata ambao walivuliwa nyadhifa zao na kubaki kuwa
wanachama wa kawaida, ni makatibu wa kata tisa, wenyeviti wa kata nane na
katibu mwenezi mmoja wa kata, wote wa Wilaya ya Babati Mjini.
Na:-Mpekuzi.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment