Dr. Vicent Machinji ( Pichani )ameteuliwa kuwa Katibu
Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kupitishwa na
Baraza Kuu la CHADEMA, katika kikao chake kilichokaa jijini Mwanza,jana March 12,2016.
Katika Kikao
hicho cha Baraza Kuu kilichodumu hadi saa
nne usiku, Mwenyekiti wa Chadema Taifa,Bw.Freeman Mbowe alitangaza jina la Dk. Machinji na kuungwa
mkono na wajumbe wa baraza hilo, hivyo anajaza nafasi iliyoachwa na Dk.
Willibrod Slaa, aliyejienguwa ukatibu mkuu wa chama hicho.
Jina la Dk.
Machinji halikuwa miongoni mwa wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wanatarajiwa
kumrithi Dk. Slaa kwani waliokuwa wanatabiriwa kukatia kiti hicho ni Salum Ally
Mwalimu, Frederick Sumaye, Benson Kigaila, John Mnyika, Dk. Marcus Albanie na
Prof. Mwesiga Baregu.
Nafasi ya
Katibu wa CHADEMA ilikuwa wazi tangu Dk. Slaa alipoondoka Chadema muda mfupi
baada ya chama hicho kumpitisha Edward Lowassa aliyetokea CCM kuwa mgombea
urais wa chama hicho na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA).
|
No comments:
Post a Comment