|
Kigogo mmoja
katika Kituo cha Polisi Kachwamba, wilayani Chato, mkoani Geita, anadaiwa
kumjeruhi vibaya askari mwenzake baada ya kumshambulia kwa chupa ya bia wakiwa
kwenye baa.
Kituo hicho
cha polisi kipo kata ya Kachwamba, nje ya makao makuu ya wilaya ya Chato,
lakini wakati tukio hilo likifanyika
kigogo huyo alikuwa Chato mjini.
Askari
aliyejeruhiwa, PC Deus Sigera wa kitengo cha upelelezi katika kituo cha polisi
Chato, amedaiwa kujeruhiwa kwenye paji la uso pamoja na shavuni na eneo la
mdomo aliumia vibaya.
Tukio hilo
lilitokea usiku wa kuamkia juzi wakati polisi hao wakipata kinywaji kwenye baa
moja iliyopo Chato mjini.
Mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo na aliyeamulia ugomvi huo kabla ya kutakiwa kwenda
kutoa maelezo polisi, Sunday Baregu, ambaye pia ni ofisa wa Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Chato, amesema kuwa wawili hao walianza kwa kujibizana kwa
maneno makali.
Alisema
baada ya majibizano hayo, kigogo huyo wa polisi alichukua chupa ya kinywaji
alichokuwa akikitumia kisha kumshambulia mwenzake usoni na shavuni kabla ya
kusaidiana na wasamaria wema kuamua ugomvi huo na kumwahisha hospitali kwa
matibabu.
“Ni kweli
niliamulia ugomvi huo na baadaye kuongozana na aliyejeruhiwa kwenda kutoa
maelezo polisi na kupewa PF3 (hati ya matibabu), lakini kwa taarifa zaidi labda
liulize Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kwa kuwa mimi siwezi kulizungumzia hilo,”
alisema.
Hata hivyo,
habari kutoka vyanzo mbalimbali zinaarifu kuwa
baada ya tukio hilo kigogo huyo alikamatwa na kuswekwa mahabusu wakati
mwenzake, PC Deus akiendelea kupata matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya
Chato.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Latson Mwabulambo, alipoulizwa kuhusu tukio hilo
alisema bado hajapokea taarifa rasmi kutoka kwa wasaidizi wake na kwamba
wanaendelea na upelekezi wa tukio hilo.
Aidha,
alidai kuwa hakuwa ofisini kwake kwani alikwenda kata ya Manyovu Runzewe kwa
shughuli za kikazi.
Source:-Nipashe.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment