|
Chama cha
Wananchi (CUF) kimesema ikitokea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad ameshinda kwa kupigiwa kura na akaibuka
mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20,2016
hatakwenda kuapishwa.
Kimesema
kuna uwezekano mkubwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ikaweka jina la Maalim,
wawakilishi na madiwani katika karatasi za kupigia kura na kusisitiza, ikitokea
hivyo na wagombea hao wakapigiwa kura, wote hawataenda kuapa.
“Kama
wagombea wetu wakichaguliwa na ZEC ikawatangaza washindi itakuwa ni kazi bure.
Pia, CUF hatutakwenda mahakamani kufungua kesi ya kikatiba kupinga hatua ya
mwenyekiti wa ZEC kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,2015” Kaimu Katibu
Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui aliwaambia waandishi wa habari jana.
Oktoba 28,
mwaka jana2015, mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi wa
rais, wawakili shi na madiwani kwa maelezo kuwa sheria na kanuni zilikiukwa na
baadaye kutangaza Machi 20,2016 kuwa siku ya kupiga kura upya.
Mazrui
alisema licha ya CUF kuiandikia barua ZEC, ikitaka wagombea wake wote
kuondolewa katika orodha ya karatasi ya kupigia kura, kuna uwezekano mkubwa wa
majina hayo kutoondolewa.
“... Sisi
tumeshaipelekea ZEC barua 54 za wawakilishi na madiwani walioshindwa au
kushinda katika uchaguzi wa Oktoba 25 na kuwaeleza kuwa wawaondoe katika
karatasi za uchaguzi wa marudio.
"Hata
kama wananchi watamchagua Maalim Seif kwa asilimia 90 hawezi kwenda kuapishwa.
Kufanya hivyo ni sawa na kukataa kula nyama ya nguruwe lakini mchuzi wa nyama
hiyo unaunywa.”
Mazrui
ambaye alitangazwa mshindi wa uwakilishi wa jimbo la Mtopepo, kabla ya kufutwa
kwa matokeo hayo alisema, “Hatuna shida na uchaguzi wao, tumekosa nini mpaka
tuwe na shida nao?”
Alisema CCM
inadhani kwamba CUF itajitosa kushiriki uchaguzi huo wa marudio katika dakika
za mwisho; “wanachotakiwa kujua ni kwamba hatuingii katika uchaguzi wao wawe na
amani yote.”
Akizungumzia
kauli ya Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu kwamba CUF walipaswa
kupinga kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi, siku 14 baada ya kutangazwa, Mazrui
alisema kauli hiyo imedhihirisha kuwa hata wakienda mahakamani hakuna haki
itakayotendeka.
“Ameshatoa
hukumu kabla hata kesi haijafunguliwa. Muda wa siku 14 aliousema unahusu ukomo
wa kupeleka kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu. Kesi ya uchaguzi msingi wake mkubwa
ni uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi ambao CUF na wajumbe wateule hatuna tatizo
nao,” alisema.
“Hakuna
anayetaka atangazwe mshindi kati ya wagombea wote wa CUF kwa kuwa walitangazwa
kihalali na wasimamizi wa uchaguzi na kupewa vyeti.
"Aliyehujumu
uchaguzi si ZEC ni Jecha. Sisi kesi tunayoweza kufungua ni ya kikatiba si
kupinga matokeo na kesi ya kikatiba haina muda wa kufungua kwa mujibu wa Katiba
ya Zanzibar.”
Alisema
kutokana na kauli ya Makungu, CUF imewashauri wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
waliokuwa na nia ya kupeleka shauri mahakamani kuachana na wazo hilo kwa
maelezo kuwa Jaji Makungu ameshaandaa hukumu na kuisoma hadharani.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment