|
Waziri wa Nchi,Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala bora,Bi.Angella Kairuki amemsimisha kazi Muu wa Chuo cha Utumishi wa
Umma nchini,Bw. Said Nassoro kutoka na uzembe ulioisababishia Serikali hasara
ya shilingi Bilioni 1.
Vilevile
Waziri Kairuki amewasimamisha kazi Mkuu
wa chuo hicho tawi la Dar es salaam,Bw.Joseph
Mbwilo na Bw.Silvanus
Ngata ambaye naye ni Mkuu wa chuo hicho tawi la Tabora.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo,February 22,2016, Jijini Dar es Salaam,Waziri
Kairuki amesema amefikia hatua hiyo ya kuwasimamisha kazi watumishi hao baada
ya kubaini utendaji usioridhisha katika vyuo hivyo.
Amesema Nassoro
amemsimisha kazi baada ya kushindwa kuwasimamia watumishi wa chini yake
katika chuo hicho.
“Mwaka
2011 hadi 2013 ,Bwana Silvanus
Ngata aliongeza gharama za ujenzi wa jengo la chuo hicho tawi la Mtwara tofauti na fedha iliyokuwa imepangwa.
"Chakushangaza,
huyu Nassoro ambaye ni mkuu wao, baada
ya kugundua kosa hilo alishindwa kumuwajibisha na badala yake aliamua
kumhamishia tawi la chuo cha Tabora. Sasa mimi nawasimamisha kazi wote
."Amesema Kairuki
Pia Waziri
Kairuki amesema amemsimamisha Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za
chuo.
“Huyu Mbwiro
kwa mwaka 2013 alitumia vibaya fedha za ada za wanafunzi kiasi cha bilioni 1 ,lakini licha ya
ubadhilifu huo, Nassoro alimteua bwana Mbwiro kuwa Kaimu mkuu wa chuo kwa
upande wa fedha." Alisema Waziri Kairuki.
Wakati
Waziri Kairuki akitumbua majipu hayo,mmoja wa watendaji hao,Said Nassoro
alikuwepo kwenye mkutano huo na wanahabari huku akiwa hajui kinatakachotokea.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment