![]() |
|
Wakati Rais Dk. John Magufuli akitarajia kutangaza
safu ya wakuu wa mikoa na wilaya wapya, imebainika
wapo zaidi ya 20 ambao watatemwa kutokana na sababu mbalimbali za utendaji.
Habari za
kuaminika zinasema miongoni mwa wakuu wa
mikoa watakaoachwa wamo walioshindwa kutatua kero sugu zikiwamo za mapigano ya
wakulima na migogoro ya ardhi ambayo kila kukicha imesababisha watu kadhaa
kufariki dunia.
Kwa mujibu
wa taarifa hizo, pia wamo wakuu wa mikoa
ambao wanaweza kuachwa kutokana na kuwa na umri mkubwa na wanaonyesha
wazi hawawezi kwendana na kasi ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano
ambayo inatumia falsafa ya Hapa Kazi Tu.
Habari hizo
zinasema wapo wakuu wa mikoa ambao wameshindwa kutatua migogoro ya ardhi katika
maeneo yao kwa zaidi ya miaka 10 hadi 15 na kusababisha vurugu kuibuka kila
wakati.Miongoni mwa mikoa iliyokithiri kwa migogoro hiyo ni Morogoro, Tanga na
Manyara.
“Wapo wakuu wa mikoa ambao hawatarudi kutokana na rekodi za
matukio, wapo ambao kwenye maeneo yao
migogoro imedumu kwa zaidi ya miaka 10 na kuendelea, sasa viongozi wa
aina hii unadhani watabaki kweli kwenye Serikali?
Chanzo hicho kilisema pia kuwa wengine ambao wako
hatarini kutemwa ni wale wenye umri mkubwa ambao kwa namna moja au nyingine
wanapaswa kustaafu.
Kuhusu wakuu
wa wilaya, chanzo hicho kilisema hakuna tofauti na wakuu wa mikoa kwa vile kila
mmoja atapimwa kutokana na namna alivyoweza kusimamia majukumu ya Serikali
tangu alipoteuliwa.
Hivi karibu
Rais Magufuli, alisema wakuu wa mikoa na wilaya wajiandae kuwajibika endapo
maeneo wanayoongoza yatakuwa na ukosefu wa chakula na kusababisha wananchi
kukumbwa na njaa wakati maeneo mengi ya nchi yamepata mvua ya kutosha.
Mikoa ambayo
imekuwa ikikumbwa na njaa mara kwa
mara ni pamoja na Mara, Iringa,
Dodoma,Tanga na Shinyanga.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
|
Monday, February 22, 2016
UTEUZI WA RAIS TANZANIA:-Rais Magufuli Kuwatema Wakuu wa Mikoa 20 .
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment