|
Katika enzi
za leo
Siku ya
Wapendao si Sikuu Rasmi nchini Marekani. Watu huenda makazini kama kawaida,
hata hivyo kama zilivyo Siku Kuu nyingi nchini humu, nayo pia imekumbwa na
kimbunga cha biashara tangu pale Hallmark walipoanzisha kuzalisha kadi zao kwa
wingi.
Hii ni siku ya pili kwa ukubwa wa mauzo katika mwaka baada ya siku ya
Christmas.
Inakadiriwa
kuwa mauzo ya kadi hizo katika siku hiyo hufikia zaidi ya Dola Billioni 15.
Baadhi ya watani wanasema kuwa "iwapo sherehe za siku ya Wapendanao
zitapigwa marufuku nchini Marekani, basi shirika la Hallmark litafilisika"
Biashara
nyengine inayochangamka katika siku hiii ni ya maua. Tani za maua huuzwa katika
siku hii, na baadhi ya wauza-maua huajiri wafanyazi wa kiasi wiki moja kabla ya
siku hii ili kukabiliana na ongezeko la wateja.
Waridi ni nembo ya pili maarufu
katika siku hii baada ya ile ya moyo.
Mbali na
biashara hizo mbili, kuna zawadi aina kwa aina ambazo watu huwanunulia wale
wawapendao, zikiwemo pipi, chakileti, na vitu vyengine vya kula na kunywa
ambavyo ama hutengenezwa katika umbo la "moyo" kama ishara ya mapenzi,
au kufungwa katika vifurushi vilivyopambwa katika mfumo kama huo.
Siyo
Hallmark tu wanaofaidika katika siku hii, bali biashara nyingi mauzo yao
huongezeka khususan mikahawa ambayo watu wanaotaka kudhirisha mapenzi kwa
wapenzi wao hujazana katika sehemu hizo na kudhihirisha mapenzi ya hali ya juu
kwa kuagizisha milo ya fakhari.
Kwa ujumla
Waswahili wanasema "Mtu hujikuna ajipatapo". Kwa hivyo, kuna wale
ambao huwanunulia wapenzi zawadi khafifu kama vile kadi yenye thamani ya chini,
na kendelea mpaka kufikia vito vya thamani, magari, majumba na sema upendavyo.
Nchini
Marekani, Canada na kwengineko, baadhi ya maskuli huandaa tafrija maalum za
Siku ya Wapendanao ambapo wanafunzi hubadilishana zawadi na marafiki zao ambazo
aghlabu huwa ni pipi, chakileti na kadi za maamkizi.
Wanaosherehekea
na Wasiosherehekea siku hii.
Ingawaje
siku hii huzalisha mabilioni ya Dola nchini Marekani, hata hivyo wako watu
ambao hawasherehekei siku hii kutokana na sababu mbalimbali.
Wale
wanaosherehekea wanaona kuwa ni siku iliyojaa upendo. "Siku ya Wapendanao
ni siku iliyojaa upendo, anga yote huwa imejaa mapenzi", anasema Angie
Bradlye, Msimamizi wa Uzalishaji katika kiwanda kimoja nchini Marekani, na
kuongeza, "ingawa mume wangu amefariki, lakini katika siku hii hujihisi
kama niko pamoja naye na moyo wangu hujaa furaha"
Naye Mae,
anaona kuwa ni fursa kwa wanaume kudhihirisha mapenzi kwa wapendanao. "Ni
siku muhimu kwa wanaume kudhihirisha mapenzi kwa wanawake wawapendao"
alisema.
Kwa upande
wa wale wasiosherehekea siku hii nao pia wana sababu zao.
Scotty ni
Mmarekani mwenye asili ya Afrika na anasema "Mimi siadhimishi siku hii kwa
sababu ni siku kuu iliyotengenezwa na Wazungu tu kwa ajili ya kujipatia pesa
kutokana na mauzo ya biashara zao"
Hata hivyo,
Blue, ni mwanamke wa Kizungu, lakini hasherehekei siku hii akisema "Huu ni
upuuzi mtupu, si chengine chochote ispokuwa wanawake wasiokuwa na shukurani
kujipatia zawadi wasizostahiki kutoka kwa mabwana zao"
Wengine huwa
hawasherehekei kwa sababu hawana wapenzi wa kusherehekea nao, kama ambavyo
Kendra Simpson kutoka Jimbo la Karolina Ya Kusini aliiambia Swahillivilla :
"Mimi sisherehekei kwa sababu sina mpenzi kwa sasa, kama nina mpenzi na
anapenda kuadhimisha siku hii, basi nitaingia naye pumbaoni".
Hata hivyo alisisitiza
kuwa kila siku inapaswa kuwa siku ya mapenzi kwa wapendao, na siyo siku hii
moja tu.
Rai hiyo
inaungwa mkono na Bi LaToya Bragg wa jimbo la Ohio, ambaye anasema "ni
jambo la kushangaza kuona watu wanahemkwa na kupoteza mapesa katika siku hii
moja, wakati ambapo mapenzi yanatakiwa kudumu kwa muda wote ambao watu
wapendanao huwa pamoja katika uhai wao"
Athari mbaya
za Kijamii.
Bi LaToya
aliyeandika kitabu kwa jina "The Heart Of Me" pia haoni sababu ya
kuadhimisha siku hii katika mfumo wake wa sasa kwa vile unaleta athari mbaya za
kijamii.
"Kuna watu wengine hali zao za kiuchumi siyo nzuri, kwa hivyo
hawawezi kunnuua zawadi kwa wapenzi wao, na hivyo wapenzi wanaokosa zawadi
kutoka kwa wapenzi wao, hujihisi duni mbele ya wenzao"
"Aidha
huleta athari za kiuchumi kwa watu wenye kipato cha chini kwa kujikalifisha
kuwanunulia wapenzi wao zawadi wazipendazo ambazo wakati mwnengine ziko nje ya
uwezo wao, almradi tu na wao waonekani ni watu katika jamii"
Mbali na
umaarufu wa siku hii, hata hivyo uchunguzi mdogo uliofanywa na Swahilivilla
umeonesha kuwa, idadi kubwa ya watu hawajui asili, chimbuko na maana ya Siku ya
Wapendanao.
Kristy, ni afisa wa mapokezi na usafirishaji katika Shirika moja la
vifaa vya magari anasema: "Ninavyojua siku hii ni ya wanaume kuwanunulia
zawadi wapenzi wao, na kwa wanaume siku yao ni ile inayoitwa 'sweetest hearts
day'.."
Naye Amanda Waleker anasema: "Sijui chochote
kuhusu asili ya siku hii, watu wanasherehekea na kuadhimisha, lakini mimi si
katika mambo yangu" |
No comments:
Post a Comment