|
Serikali
imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwezi huu wa February ,tofauti na
zilizokuwa zikukusanya hapo awali za bilioni 850 kwa kipindi cha mwezi mmoja na
kuzielekeza fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Takwimu hizo
zimetolewa Jana ,February 22,2016, jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Dkt. Servacius Likwelile wakati
akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha mwezi Februari mwaka huu,2016.
Dkt. Likwelile
amesema ‘kati ya fedha hizo ,sekta ya elimu imepewa shilingi bilioni 18.7 kwa ajili ya utekelezaji wa utoaji wa elimu
bure kwa wanafunzi wa shule za awali hadi kidato cha Nne ambapo fedha hizo ni
kwa ajili ya malipo ya ada,chakula pamoja na ruzuku‘.
‘Mkoa wa Dar es salaam imeongezewa shilingi bilioni 2 ili kupanua
uwezo wa udahili kama Rais alivyoahidi katika mkutano wake na Wazee wa Mkoa huo
na kati ya fedha hizo wakufunzi
wamepatiwa shilingi milioni 431.6 walimu walio masomoni wametengewa shilingi milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya
kufundishia, posho na nauli‘
‘ fedha
nyingine kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili
ya mishahara ya watumishi wa Umma , ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu
zimetolewa shilingi bilioni 842.1 na Mifuko ya hifadhi za Jamii zimetolewa
shilingi bilioni 81.13‘.....Unaweza kumtazama hapa Katubu Mkuu Dkt. Servacius Likwelile''.
|
Tuesday, February 23, 2016
Home
HABARI
HAPA KAZI TU:- Serikali ya Rais Magufuli yakusanya zaidi ya trilioni 1 February 2016 na kugawanywa kwenye Miradi ya Maendeleo.
HAPA KAZI TU:- Serikali ya Rais Magufuli yakusanya zaidi ya trilioni 1 February 2016 na kugawanywa kwenye Miradi ya Maendeleo.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.





No comments:
Post a Comment