EMIRATES FA CUP 2015/2016:-Manchester United usoni mwa West Ham Robo Fainali ya FA CUP. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 23, 2016

EMIRATES FA CUP 2015/2016:-Manchester United usoni mwa West Ham Robo Fainali ya FA CUP.

HAPO Jana February 22,2016,Usiku mjini Greenhous Meadow, Manchester United walifanikiwa kuifunga Timu ya Daraja la chini la Ligi 1, Shrewsbury Town, katika mchezo wa mwisho wa raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP ,kwa goli 3-0 na kwenda Raundi ya 6 ambayo ni Robo Fainali ambapo watakutana na West Ham huko Old Trafford.
Bao za Manchester United katika mchezo huo zilifungwa Kipindi cha Kwanza Dakika ya 37 kupitia Chris Smalling na Frikiki ya Juan Mata ya Dakika ya 45 huku Jesse Lingard alipiga Bao la 3 Dakika ya 61 na kuwapa Man United ushindi wa raha wa 3-0 ambao umeondoa presha kwa Meneja wao, Luis van Gaal, anaesakamwa hasa kwa mwenendo wa matokeo mabaya.
Alhamisi,February 25,2016, Manchester United wako kwao Old Trafford kurudiana na FC Midtjylland wakitakiwa kupindua ushindi wa Wadenishi hao wa Bao 2-1.

 EMIRATES FA CUP 2015/2016 -DROO YA ROBO FAINALI

Manchester United v West Ham

Arsenal au Hull City v Watford

Everton v Chelsea

Reading v Crystal Palace

** Mechi za Robo Fainali zitachezwa Wikiendi ya Machi 12,2016.


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad