EMIRATES FA CUP:- Mabingwa Watetezi Arsenal hoi kwa Hull City. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 21, 2016

EMIRATES FA CUP:- Mabingwa Watetezi Arsenal hoi kwa Hull City.

Mabingwa Watetezi wa FA CUP Arsenal itabidi waende huko KC Stadium kurudiana na Hull City baada ya Jana February 20,2016 kutoka Sare 0-0 Uwanjani Emirates katika Mechi ya Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP.
Kila Timu ilifanyika mabadiliko makubwa katika Vikosi vyao vilivyocheza Mechi zao zilizopita kwa Arsenal kubadili Wachezaji 9 na Hull City 10 lakini Arsenal wakashindwa kuipenya ngome ya Hull huku Kipa wa Vinara hao wa Daraja la chini la Championship wakijilinda imara kwa Kipa wao, Eldin Jakupovic, kuokoa Bao kadhaa za wazi.
Katika Mechi nyingine za Raundi ya 5 ya FA CUP zilizochezwa jana,Jumamosi Readuing, inayocheza Championship, iliitwanga West Brom ya Ligi Kuu Bao 3-1 baada ya kutoka nyuma kwa Bao la Dakika ya 54 la Darren Fletcher na kuibamiza 3 , kupitia Paul McShane, Dakika ya 59, Michael Hector, 72, na Lucas Piazon, 94.

Nao Watford wameitungua Leeds United 1-0 kwa Bao la kujifunga mwenyewe Scott Wootton la Dakika ya 53 huku Bournemouth akifungwa 2 – 0 na Everton,kwa goli za Ross Barkley dakika ya 56 na Romelu Lukaku dakika ya 76’.

EMIRATES FA CUP 

Raundi ya 5

Jumapili Februari 21

1700 Blackburn v West Ham   
     
1800 Tottenham v Crystal Palace 

1900 Chelsea v Man City  
            
Jumatatu Februari 22

2245 Shrewsbury v Man United    

Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630  Or  +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad