Beki wa
kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa
Yanga Juma Abdul
Bao la
kwanza la Yanga SC limefungwa na Donald Ngoma dakika ya 39 baada ya Hassan
Kessy kutoa pasi fupi kwa golikipa wake Vicent Agban ambayo ilinaswa na
mzimbabwe huyo na kuwekwa kambani mapema kipindi cha kwanza.
Yanga
walipata bao la pili kutoka kwa nyota wa mchezaji wa zamani wa Simba Amis
Tambwe dakika ya 72 kipindi cha pili.
|
Adbi Banda
akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa
kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano.
Rekodi
unazotakiwa kujua
Yanga SC ndiyo timu ya kwanza kuifunga Simba
tangu iwe chini ya kocha Jackson Mayanja tangu kocha huyo atangazwe kuchukua
mikoba ya Dylan Kerr.
Simba SC ilikuwa haijafungwa zaidi ya goli
moja tangu iwe chini ya Mayanja, Yanga wamekuwa timu ya kwanza kuifunga Simba
zaidi ya goli moja baada ya kuifunga bao 2-0.
|
Raha ya
ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba SC.
Yanga SC inapanda kileleni mwa ligi kwa mara
nyingine baada ya kufikisha pointi 46 ikiwa imecheza michezo 19 huku Simba
SC yenye pointi 45 sawa na Azam FC ikishuka hadi nafasi ya tatu ikitofautiana kwa
wastani wa magoli na Azam FC.
|
Raha ya
ushindi, mashabiki wa Yanga SC wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba SC.
Yanga SC inapanda kileleni mwa ligi kwa mara
nyingine baada ya kufikisha pointi 46 ikiwa imecheza michezo 19 huku Simba
SC yenye pointi 45 sawa na Azam FC ikishuka hadi nafasi ya tatu ikitofautiana kwa
wastani wa magoli na Azam FC.
|
Mashabiki wa
Simba SC wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa
jadi Yanga SC
Simba
SC itakuwa mwenyeji wa Mbeya City March 6, 2016 kwenye mchezo wao ujao wa VPL 2015/2016
kwenye uwanja wa taifa.
Yanga
SC wataialika Mtibwa Sugar kwenye mchezo unaofuata katika liga, mchezo huo
utapigwa kwenye uwanja wa taifa February 24, 2016.
Matokeo ya
michezo mingine iliyopigwa leo kwenye viwanja mbalimbali
Mgambo JKT
1-1 Tanzania Prisons
Stand United
1-1 JKT Ruvu
Mbeya City
0-3 Azam FC
Toto
Africans 1-1 Kagera Sugar
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment