Baraza la
mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka
2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.
Akitangaza
matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa
jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani
wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa
68.33%.
Msonde
amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na
asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na
wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
Amesema kwa
upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa
na mwaka 2014.
Aidha kwa
upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa 31,951 sawa
na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12)
waliofaulu mwaka 2014.
Kwa upade wa
ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Msonde
amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la
pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia
13.56.
Aidha
waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja
la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
Watahiniwa
waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa
na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338 sawa
na asilimia 19.63.
Amesema kwa
upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu kabisa ni wa
somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa
ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.
Matokeo hayo
yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa
alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi hivi karibuni.
|
No comments:
Post a Comment